HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 24, 2022

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO (DRC)

 


Na Mwandishi wetu.
WAZIRI wa Kilimo amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika kuendeleza sekta ya kilimo hususan katika nyanja za utafiti, kubadilishana utaalamu na kuimarisha soko la mazao mbalimbali.

Waziri Bashe amesema hayo wakati akizungumza na ujumbe kutoka DRC ulioongozwa na Gavana wa Jimbo la Katanga, Jacques Kyabula Katwe ambao upo nchini kwa ziara ya siku tatu kufuatilia ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ushirikiano katika Kilimo.

Bashe amesema, Tanzania imejipanga kuimarisha upatikanaji wa chakula nchini DRC ambapo katika kuhakikisha kila upande unanufaika na biashara ya chakula kupitia maghala hayo wafanyabiashara wa Congo watakuwa wakinunua kutoka kwenye maghala na kwenda kuuza kwa wananchi.

“Katika kuhakikisha Congo inanufaika na mazao mbalimbali kutoka Tanzania serikali inaendelea kuimarisha ujenzi wa maghala mbalimbali ambapo kwa sasa Tanzania kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) imejipanga kutoa mafunzo ya kiutaalamu kwa wataalamu wa kilimo kutoka ukanda wote wa Mashariki ya Congo pamoja na kuiwezesha Congo

Amefafanua kuwa Tanzania kwa kushirikiana na DRC italisha bara zima la Afrika kutokana na ukubwa wa ardhi inayopatikana kwenye nchi hizo huku zikiwa na kiwango kikubwa cha maji ya kutosha kwa kilimo cha umwagiliaji.

Amesema Tanzania itaingia makubaliano ya kisheria na ukanda mzima wa Mashariki mwa Congo katika ufanyaji wa shughuli za kilimo.

Amesema, “Tanzania inaenda kufungua maghala mengi zaidi kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya aina mbalimbali ambayo yanahitajika zaidi nchini DRC na wafanyabiashara wa Tanzania hawataingia mitaani kuuza mazao ila wakongo wenyewe watanunua kwenye maghala na kwenda kuuza kwa watu wao”

Kwa upande wake Gavana wa Jimbo la Katanga, Jacques Kyabula Katwe amesema kuwa Jimbo la Katanga linavutiwa na uwezo wa Tanzania katika shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo na ina Imani kuwa ushirikiano kati ya jimbo la Katanga utaenda kuimarisha maisha ya watu wa jimboni mwake.

Amesema atahakikisha kuwa biashara ya chakula kutoka Tanzania inazidi kuimarika kila kukicha na kuwa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwanufaisha wakulima wa Katanga huku akiishukuru serikali kwa kuwa msaada mkubwa kwa biashara ya chakula kwa nchi ya Congo hususan Jimbo la Katanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad