HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2022

RC Kindamba ashuhudia utiaji saini wa mikataba ya maji ya Bilioni 12.6

 Njombe

SERIKALI kupitia mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Njombe (NJUWASA) imesaini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya maji miwili yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 12.6

Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe na wajumbe waliohudhulia katika hafla hiyo fupi,Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo MhandisiJohn Mtyauli amesema kukamilika kwa ujenzi wa miradi hiyo kutaongeza idadi ya wakazi wanaofikiwa na huduma ya maji kutoka 67.9% hadi kufikia 85%

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba amewaagiza wakandarasi watakaokwenda kutekeleza miradi hiyo kuhakikisha ujenzi wa miradi hiyo unakamilika ndani ya muda uliopangwa.

“Nitoe Rai kwa wakandarasi kuhakikisha ujenzi wa miradi hii unakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa kuzingatia ubora uliokusudiwa ili wakazi wa Njombe waanze kunufaika na huduma ya maji”amesema Kindamba

Mradi unaokwenda kutekelezwa ni mradi wa maji wa mserereko wa Livingstone utakaotekelezwa na mkandarasi M/S PERITUS EXIM PRIVATE LTD uliokadiriwa kugharimu kiasi cha Bilioni 3,975,910,336.00 Pamoja na mradi wa maji wa kupampu na mserereko wa kutoka Lugenge utakaotekelezwa na M/S NANDHRA ENGINEERING & CONSTRUCTION LTD uliokadiriwa kugharimu kiasi cha Bilioni 8,763,890,262.86
Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo MhandisiJohn Mtyauli akisaini mkataba na mmoja wa wakandarasi mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba.
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo MhandisiJohn Mtyauli akionyesha mkataba ambao tayari umekwishasainiwa.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akikata utepe sehemu ya mikataba ya wakandarasi tayari tayari kwa ajili ya kusainiwa ili kuweza utekelezaji wa miradi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad