Benki
ya NMB imelizindua rasmi jukwaa la kuwawezesha vijana la “GO na NMB”
Visiwani Zanzibar na kusema iko tayari kusaidia kuwajenga kiuchumi na
kuwakwamua kifedha kwa kuwahudumia kidigitali, kuwakopesha na kuwapa
elimu ya fedha.
Akiuelezea
mpango huo wenye manufaa lukuki mbele ya mgeni rasmi aliekuwa Makamu wa
Pili wa Rais, Ndugu – Hemed Suleiman Abdulla, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB – Bi Ruth Zaipuna, alisema benki hiyo iko vizuri
kiteknolojia kusaidia kuyabadilisha maisha ya vijana wa Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla.
Bi.
Ruth alisema jukwaa la Go na NMB limekuja na fursa mbalimbali kwa
vijana ikiwemo; Mikopo ya vitendea kazi mfano mkopo wa pikipiki
(Mastaboda), boti (Mastaboat) na mingine mingi. elimu ya kifedha na
ujasiriamali, bima mbalimbali ikiwemo bima ya simu bila malipo ya ziada,
fursa za ajira kupitia programu ya uongozi kwa wanafunzi waliohitimu
chuo (Management Trainee)
Lakini
pia, kuwapa elimu kuhusu huduma za kidigitali kama NMB Lipa Mkononi,
NMB Mshiko Fasta na NMB Pesa Wakala ambayo mbali ya matumizi ya kuweka
na kutuma fedha, inaleta ajira kwa vijana na wengine kutimiza ndoto zao.
Kupitia
masuluhisho ya jukwaa hili, Benki ya NMB imejipanga kuwafikia vijana
wote wa zanzibar, kuanzia wanafunzi mpaka vijana wenye shuguli za
uzalishaji kwenye sekta zote za uchumi na litawahamasisha vijana
kujiwekea akiba na kuweka mikakati ya kuwa na shughuli za uzalishaji na
kuwahakikishia vipato wakati wote
Katika
hotuba yake, Makamu wa Pili wa Rais, Ndugu – Hemed Suleiman Abdulla
alisema, jukwaa hili linaendana na juhudi za Serikali za kutatua
changamoto zinazowakabili vijana visiwani humo, na limekuja wakati
muafaka, kwani ni uwekezaji wenye tija kwa sababu kuwainua vijana
kifedha na kiuchumi kutasaidia sana kukabiliana na tatizo la ukosefu wa
ajira.
Aidha,
aliwapongeza NMB kwa hatua hii waliyofikia katika kuhakikisha
wanawakwamua vijana pale walipo na kuwatengeneza uwezo wa kuwa na
nidhamu ya fedha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Ndugu Hemed Suleiman Abdulla akizindua huduma ya ‘Go na NMB’ visiwani Zanzibar. Wakishuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna (wa tatu kutoka kulia), Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi, Filbert Mponzi (wa pili kutoka kulia) Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Shaame na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja – Rashid Simai Msaraka.
No comments:
Post a Comment