HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2022

Maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki kati ya Jiji la Dar na Humburg, Kujadili mabadiliko ya tabianchi

 

Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki  wa mini Kati ya Jiji la Dar es Salaam na Harmburg Dkt.Sylvia Luambo akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo.

Na Humphrey shao, Michuzi Tv
MIONGONI mwa Shughuli zitakazofanyika katika Maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki wa miji kati ya Jiji la Dar es Salaam na Humburg wageni zaidi ya 30 wanatarajia kuja nchini na kuja kujadili mambo mbalimbali ikiwemo changamoto na fursa zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi kwa manufaa ya wananchi wa majiji hayo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki wa miji kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg, Dkt.Sylvia Ruambo amesema wadau hao kutoka katika pande hizo mbili wanatoka katika taasisi mbalimbali za serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi.

Amesema kupitia fursa hii wameona kuna umuhimu wa wao kukutana na kufanya majadiliano hayo ikiwa ni sehemu za juhudi za kushirikiana na serikali katika jitihada zake za jukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.


"Urafiki kati ya majiji hayo umechangia na kusaidia kuboresha huduma katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya afya, mazingira, elimu, utafiti na utamaduni,alisema na kuongeza

"Aidha majiji hayo yamewasaidia wataalamu wake na wananchi kufanya ziara za kujifunza, kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi na utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,"alisema Dkt.Ruambo

Alisema katika kipindi cha miaka 12 ya urafiki huo wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Ardhi na Jiji la Humburg wamekuwa mstari wa mbele katika uandaaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kufanya utafiti kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kukabiliana nazo kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mazingira.

Amesema urafiki wa jiji la Dar es Salaam na jiji la Humburg ulianza rasmi Julai 2010 baada ya majiji hayo kutia saini hati ya makubaliano ya kuanzishwa kwa urafiki huo hivyo maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki wa majiji unatarajiwa kuwakutanisha wadau wengi kutoka katika sekta mbalimbali ambao watashauriana pia kuhusu njia bora ya kuimarisha urafiki huo na kuongeza idadi ya watu wanaonufaika na fursa zitokanazo na uhusiano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad