Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa na Balozi wa
Marekani nchini Tanzania Donald Wright wameongoza zoezi la kihistoria la
kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kufunguliwa kwa safari za moja kwa
moja za Usafiri wa anga baina ya nchi hizo mbili.
Hafla hiyo ya kusaini mkataba huo ilivyohudhuriwa na
viongozi na wadau mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi Gabriel Migire, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA)
Musa Mbura.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo Waziri Mbarawa alisema maboresho hayo ya itifaki ya
mkataba ambao awali ulisaini Agosti mwaka 2000 ni sehemu sasa ya fursa
mpya za usafiri baina nchi mbili , ongezeko la abiria pamoja na kukuza
biashara na uchumi. Na kuongeza kuwa sasa anaamini kwa fursa hiyo
shirika la ndege nchini(ATCL) na mashirika mengine ya ndege
yaliyosajiliwa nchini yataichangamkia.
"Kufikiwa kwa azma hiyo ya kuwa na usafiri wa anga wa moja kwa moja
kati ya Marekani ni matokeo chanya ya ziara ya Mhe.Rais Samia Suluhu
Hassan nchini Marekani na uzinduzi Filamu ya Royal Tour" Alisema Mbalawa
Kwa
upande wake Balozi Wright alisema hafla hiyo inahitimisha safari ya
miaka takribani 22 ya Kihistoria tangu Marais wa Tanzania na marekani ambao ni Benjamin Mkapa na Bill
Clinton kutia saini mkataba wa ushirikiano wa usafiri wa Anga Agosti
mwaka 2000 nchini Tanzania sambamba na mazungumzo baina ya Rais Samia na
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris Aprili 15,2022 nchini Marekani
na Sasa ndoto ya kuwa na anga la pamoja inafikiwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu TCAA Hamza Johari alisema wao kama wataalam
Sasa jukumu lao ni kukamilisha masharti baina ya pande hizo mbili na
hatimaye kufungua rasmi fursa na kuongeza kuwa mkataba huo ni wa aina
yake kwani unaruhusu aina mbalimbali za ndege, miruko mingi na hata
uwezo mbalimbali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia)
pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald
Wright(kushoto) wakionesha itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) pamoja na Balozi wa
Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright(kushoto) wakisaini itifaki
ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia)
pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald
Wright(kushoto) wakibadilishana itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa
habari pamoja na wadu mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakati hafla ya
kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa
Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright.
Balozi
wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright akizungumza na wadau
mbalimbali wa Usafiri wa Anga pamoja na waandishi wa habari wakati
hafla ya
kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA),Hamza S.Johari akitoa
neno la shukrani kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania pamoja na
Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi
la kutia saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya
Tanzania
na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Usafiri wa Anga wakifuatilia zoezi la utiaji saini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa(kulia) akiagana na Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald
Wright(kushoto) mara baada ya kumaliza zoezi la kusaini itifaki ya maboresho ya Usafiri wa Anga baina ya Tanzania
na Marekani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment