HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2022

KUNUSURU MIUNDOMBINU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

 

KuliaBw. Raymond Mndolwa, akionesha sehemu ya daraja la mto Mvomero, halipo katika picha, lililoharibiwa vibaya na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi pamoja na shughuli za kibinadamu. wengine katika pichani watumishi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mvomero na Ofisi za Tume ya taifa ya Umwagiliaji Mkoani Morogoro.

Picha ikionesha sehemu za kingo za mto Mvomero zilivyoharibiwa vibaya na shughuli za binadamu.

Picha ikimuonesha Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiwa na wataalam katika kikao cha pamoja, kilichofanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero kabla ya kwenda kutembelea Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Msufini.


Na Mwandishiwetu -Mvomero
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa, amewaasa wakulima nchini kutunza vyanzo vya maji kwa kutokufanya shughuli za kibinadamu hususani za kilimondaniyamitasitini (60) ilikunusuru kuharibika kwa kingo za mito unaopelekea uharibifu wa Miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji.

Bw.Mndolwa ameyasema hayo mapema alipokuwa akizungumza na wakulima wa skimu ya Umwagiliaji Msufini iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, inayotumia maji kutoka mto Mvomero kama chanzo cha maji ya kilimo cha Umwagiliaji, ambapo ameshuhudia uharibifu mkubwa uliofanyika kutokana na shughuli za kilimo zisizorasmi.

Aliwashauri viongozi wa S erikali yakijiji kushirikiana kulinda vyanzo hivyo vya maji kwa manufaa ya kila mwananchi na aliendelea kusema “Hatulindi vyanzo vya maji yakunywatuu, hata vya kilimo na kuzuia uharibifu unaofanywa na binadamu wenzetu, asili inaharibiwa na binadamu.”Alisisitiza

Bw. Mndolwa aliagiza wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji nawataalam kutoka Halmashauri kufanya mapitio ya mto na chanzo nakuona athari iliyotokana na mafuriko yaliyopita katika mto huu.

Katika zoezi hilo wataalam watatakiwa kuja na mapendekezo yanini kifanyike ili kurekebisha athari za mafuriko hali itakayopelekea skimu ya Msufini kuanza kufanya kazi.

Aliongeza kuwa, kitachofanyika kwa sasa nikutengeneza chanzo kinachopeleka maji katika skimu hiyo matengenezo ambayo yataridhisha pande zote ikiwa ni pamoja na serikali na watumiaji wa skimu hiyo.

“siwezi ruhusu mkandarasi aliyefanya kazi kwa kiwango cha chini upande mwingine aje tena hapa,sababu kuna mahali kaharibu na nitamfukuza, kama kaharibu kwingine na hapa ataharibu.”Alibainisha Mndolwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundo mbinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi Ntonda Kimasa alisema, kuwa mradi huo umetengewa fedha kwa mwaka wafedha 2022/2023 kwa ajili yakuboresha miundombinu yake, hivyo mara baada ya kukamilika mapendekezo ya timu kazi ya ukarabatiwa miundombinu itaanza mara moja.

Awali, Bw. Mndolwa aliwakumbusha wakulima swala zima za kulipa Tozo na ada za matunzo ya skimu za Umwagiliaji baada ya kujengewa na kukarabatiwa kwa miundombinu hiyo.

Kwa upande mwingine aliwashauri wadau husika akitolea mfano wadau wa barabara, kilimo na wadau wengine wakae kwa pamoja ili yafanyike maamuzi sahihi na kuona namna ya kuunusuru mto mvomero kutokuacha njia yake ya asili na kupelekea kuvamia makazi ya watu.

Skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Msufini, iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro pamoja na kuathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi,imeharibiwa vibaya nashughuli za kibinadamu zinazofanyika ndani ya mita sitini, bila kuzingatia sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad