HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 17, 2022

KONGAMANO LA PENUEL 2022 KUANZA JUNI 30

 

KANISA la Living Water Centre Tanzania linakukaribisha katika Kongamano la Penuel 2022 lenye Kauli mbiu "Mavuno kwa Bwana" sawasawa na Mathayo 9:37 lenye lengo la kukujenga na kukupa maarifa ya mavuno makubwa katika kila eneo la maisha yako,njoo ukutane na Bwana wa Mavuno kupitia Neno na Mungu, pia Kusifu na kuabudu. Wanenaji ni Bishop Olam Mustapha kutoka Arusha na Apostle Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini pamoja na Wenyeji ni Apostle Onesmo na Lilian Ndegi.

Kangamano hili litafanyika Kanisa la Living Water Center Kawe, Dar es salaam jirani na Mahakama ya mwanzo Kawe.

litaaanza siku ya Alhamis tarehe 30 Juni hadi tarehe 3 Julai 2022.

siku ya Alhamis tarehe 30 Juni litaanza Saa 10 jioni hadi saa 1 usiku
~ Ijumaa saa 3 asubuhi hadi saa 1 usiku
~ Jumamosi saa 3 asubuhi hadi saa 1 usiku
~ Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 1 usiku

Waimbaji watakaohudumu ni Apostle Solly Mahlangu kutoka South Africa, Living Waters wenyeji, Seeds of Life kutoka Mwanza, The Living Sacrifice kutoka Iringa, The Fountain of Grace kutoka Dodoma, John Lihawa, Banabazambe,Women of The Kingdom kutoka Dar es salaam na wengine wengi!

Mawasiliano:
+255 743 19 66 26
+255 713 11 77 77
Hakuna Kiingilo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad