HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2022

JKT LAWAITA VIJANA KIDATO CHA SITA KURIPOTI MAKAMBINI NDANI YA SIKU TATU

 

Na Janeth Raphael - Dodoma
MKUU wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka kuripoti makambini vijana wote walioitwa kuhudhuria mafunzo ya (JKT) kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022 ambao hawajaripoti mpaka Sasa waripoti makambi ya JKT mara moja.

Taarifa hiyo imetolewa leo juni 22, 2023 na Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la kujenga Taifa, Brigedia Jenerali Hassan Mabena katika mkutano na wana habari akiwa Makao Makuu ya Jeshi ya Jeshi la kujenga Taifa Chamwino Dodoma.

Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema Vijana haoe wote wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT kuanzia leo tarehe 22 juni, 2022 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 25 juni 2022.

Aidha Brigedia Jenerali Hassan Mabena katika taarifa hiyo amesema Vijana hao wote waripoti makambi ya JKT yalio karibu na maeneo wanayoishi, Isipokuwa kambi ya Makutupora JKT iliyopo Mkoani Dodoma, CUJKT iliyopo Kimbiji Mkoani Dar ea Salaam na Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo inapokea wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical Disabilities) yenye miundombinu ya kuwahudumia watu wa jamii hiyo.

Hata hivyo Brigedia Jenerali Mabena amesema nyongeza ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2022 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2022.

Kutokana na taatifa hiyo orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa awamu ya pili, Vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, vinapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad