HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2022

JAMII YAASWA KUTOWANYANYAPAA WENYE VIRUSI VYA UKIMWI, WACHOCHEA USUGU WA DAWA

 

Picha ya pamoja ya wadau mbalimbali mara baada ya kufunga mafunzo ya kuangalia afua za kuwasaidia wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi. Semina hiyo imefanyika kwa siku nne katika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.

JAMII imeaswa kutowanyoshea vidole watu wanaotumia dawa za kufuvaza Virusi vya Ukimwi kwani wanasababisha watu hao kutokutumia dawa vile inavyotakiwa.

Hayo yamesemwa na Mkuu Mkuu wa Idara ya Masomo ya Biashara kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Daktari Omary Swalehe wakati akizungumza na Mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo, Juni 21, 2022, mara baada ya kufunga Mafunzo ya siku nne ya wadau mbalimbali.

"Unyanyapaa imekuwa ni tatizo sugu, imekuwa ni kitu ambacho kinasababisha Wagonjwa wasitumie Dawa kwa sababu hakuna mtu anapenda aonekane katika jamii kama anaumwa Ugonjwa au anatumia dawa za Kufubza virusi vya Ukimwi...

Na kujificha ficha inapelekea watu kutokutumia dozi zao kwa ukamilifu na kupelekea kuwa na Usugu wa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi." Amesema Dkt. Omary

Amesema kuwa Jamii inatakiwa kuwaangalia watu wenye Virusi vya Ukimwi kama watu wengine na kuto wanyooshea vidole pindi wanapoenda kuchukua au kutumia dawa hizo.

Amesema kuwa Jamii inatakiwa kuelemishwa ili iache kuwanyanyapaa watu wanao wanaotumia zawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi ili waweze kutumia dawa hizo bila kikwazo chochote.

Amesema katika matokeo ya utafiti wa awali imeonesha mambo mbalimbali yanachangia Usugu wa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaotumia zawa hizo ikiwemwo Umasikini, Umbali wa maeneo ya kuchukulia dawa kwa wagonjwa pamoja na kutokuwa na fedha za kujikimu wakati wanapotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi.

Amesema Matokeo ya Utafiti huo ni utafiti uliofanyika katika wakazi wa Ukonga na Gongo la Mboto jijini Dar Es Salaam. Aidha ameomba wadau mbalimbali kuwasaidia wagonjwa hao kwa kuwapa mikopo ili waweze kufanya biashara ndogo ndogo ili kujipatia kipato kitakacho wasaidia kukidhi mahitaji yao kipindi chote wanapotumia dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya Ukimwi.

Kwa upande wa serikali wameombwa kupeleka huduma za afya karibu na wananchi ili kuwapunguzia umbali wa kwenda kuchukua dawa.

Mafunzo hayo yamefadhiriwa na chuo cha KU LEUVEN cha uberigiji wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Hospitali za Serikali, Hospitali binafsi na wadau mbalimbali katika kufanya utafiti juu ya namna ya kukabiliana na Usugu wa Dawa za Kufubaza virusi vya Ukimwi.

Utafiti huo umeratibiwa na Prof. Anne-Mieke Vandamme, Prof. Nico Vandaele, Dkt. Catherine kutoka KU LEUVEN, Prof. Japheth Killewo, Prof. Raphael Sangeda kutoka MUHAS na Dkt. Omary Swalehe kutoka MUDCC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad