HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 1, 2022

Hoteli ya nyota tano ya Johari Rotana yafunguliwa tena nchini, yajizatiti kuleta mapinduzi kwenye sekta ya utalii na ukarimu

HOTELI ya nyota tano ya Johari Rotana imeanza kutoa huduma baada ya kufungwa kwa miaka miwili baada ya matumaini mengi kwa kuzingatia ufunguaji mipaka ya nchi nyingi na hali ya utalii kushika kasi katika maeneo mengi. Kutokana na kuondoa vikwazo vya usafiri , idadi ya watalii wa kimataifa wanaowasili Tanzania imekuwa ikiongezeka hali ambayo imechangia ushawishi chanya na ukuaji katika sekta ya ukarimu.

Joerg Potreck, Meneja Mkuu wa Johari Rotana, alisema: "Ufunguzi wetu umekuja wakati muafaka baada ya Tanzania kutajwa kuwa nchi inayoongoza kwa kutembelewa na watali yaani "Africa's Leading Destination" kwa mwaka 2021 na utitiri wa watalii nchini. Ni jambo la furaha kwetu wote na timu yangu imejipanga kuwakaribisha wageni wetu tena haa Johari Rotana.”

Inapatikana kwa urahisi katika eneo la MNF Square katika Mkoa wa kibiashara wa Dar es Salaam (CBD), Hoteli hii yenye mvuto wa kipkee na wa kuvutia inatoa funguo 253 ikijumuisha vyumba 193 vya hoteli vyenye ukubwa wa wastani wa zaidi ya sqm 150, na vyumba 60 vya kujitegemea vyenye samani kamili vinavyotoa mandhari nzuri ya Bandari ya Dar es Salaam na jiji lake. Vyumba, na apartment vimeenea katika gorofa 15 kuanzia ghorofa ya 13 ya mradi wa matumizi mchanganyiko wa sqm 65,000.

"Hii imeweka viwango vipya katika usanifu, muundo, teknolojia, na ubora wa huduma, katika hoteli yetu ya Johari Rotana, ambae ni hoteli yetu ya kwanza kwenye kenda ya Afrika Mashariki ambae imejizatiti kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya ukarimu. Tuna uhakika kwamba vyumba vyetu vya kulala, kumbi za vyakula na vinywaji, vifaa vya hali ya juu vya mikutano ikiwa ni pamoja na ukumbi mkubwa zaidi wa burudani nchini Tanzania yaani ballroom na huduma nyingine vitavutia wageni wetu na kuleta usindani wenye tija sokoni,” aliendelea Potreck.

Johari Rotana inatoa aina mbalimbali za mlo, ana kumbi nne maridadi, ikiwa ni pamoja na chumba cha kupumzika cha Kibo, mgahawa unaotoa huduma siku nzima wa Zafarani, mgahawa wa hali ya juu wa Kichina wa Noble House na baa ya kipekee ya Hamilton's Gastropub. Hoteli hiio pia inajivunia kuwa na ukumbi kubwa zaidi la mikutano .

Hoteli hii pia ina vyumba sita vya ziada vya mikutano na eneo la maji tiririka la kuvutia yaani water front, kituo cha biashara , ofisi daraja A, na kituo cha maegesho ya ndani, na kuifanya kuwa chaguo bora kwa wageni wa biashara na burudani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad