HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 4, 2022

DREAM- MAKERS 30 WATUNUKIWA VYETI NA TAASISIS YA MANJANO FOUNDATION

 TAASISIS ya MANJANO FOUNDATION yahitimisha Mafunzo y wiki mbili kwa Dream- Makers 30 jijini Dar es alaam leo Juni 4,2022 ambao walianza mafunzo hayo Mei 23, 2022.

Akizungumza wakati wa kuwaaga Manjano Dream Makers 30, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser amesema kuwa dream Makers wengi wapo katika tasnia mbalimbali.


"Tunafahamu Dream Makers wapo katika tasnia mbalimba lakini sisi tunataka tuone maendeleo yenu, ndio maana tunawapa barua kwaajili kutoa ahadi (Comitment letter) ili unapotoka hapa tujue una hali gani, nayo inatutia faraja kwa wasichana wengi na wanawake wakisaidia katika kusukuma gurudumu la maendeleo."

Kama mjuavyo kwa mara ya kwanza tumepata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mwanamke wa kwanza yeye anatuvutia wote, wasichana na wanawake wamshike mkono, tusibweteke, tusaidie familia." 

"Yaani hata kama Mume analeta milioni moja wewe ukaleta laki au elfu hamsini inasaidia katika kuongeza kuishi katika maisha mazuri, watoto wetu wasome vizuri na tuweze kula milo mizuri." Amesema Shekha

Amesema ukiangalia familia zetu watoto wanakosa vitamini mhimu na yeye anapigania hicho wanawake watoke kwenye utegemezi ya wazazi au Mume katika kuangalia afya ya watoto.

"Ukiangalia lita moja ya maziwa ni kuanzia elfu mbili hivyo we asichana na wanawake mnatakiwa muwe na uwezo wa kununua vitu mhimu kwa watoto na sio kutegea mtu mwingine." Amesisitiza Shekha wakati wa mkuhitimisha mafunzo ya wiki mbili kwa dream Makers 30.

Amesema kunafamilia nyingi zinashindwa kukidhi mahitaji hata ya kununua maziwa ya watoto kwa wiki mara moja ambayo ni mazuri kwa afya ya watoto katika familia  hata kama upo kwenye maisha magumu kiasi gani.

Hata hivyo Shekha amewaasa dream Makers 30 kutoa elimu waliyo ipata kwa watu watatu au zaidi kwaajili ili nao wapate kile kidogo ambacho wakipata kutoka MANJANO FOUNDATION.

Kwa Upande wa Mwakilishi wa dream Makers 30 amemshukuru Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser kwa kujitolea kuwafundisha mambo mbalimbali waliyojifunza katika taasisi hiyo.

"Mwenyezi Mungu amzidishie pale alipopunguza." Amesema

Dream Makers 30 waliohitimu leo walianza mafunzo hayo Mei 23,2022 ikiwa ni kama kawaida ya Taasisi ya MANJANO FOUNDATION kutoa elimu bure kwa wasicha na wanawake 30.

Taasisi ya MANJANO FOUNDATION imekuwa ikitoa mafunzo hayo bure tangu Mei 2015 kwa Manjano Dream-Makers 30 ikiwa program hiyo ni ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia Kipodozi cha LuvTouch Manjano.
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser  wakifurahia baada ya kuwakabidhi vyeti Dream Makers 30 leo  Juni 4,2022 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser, Dream Makers 30 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya wiki mbili. Mafunzo hayo yamehitimishwa leo Juni 4,2022 kwa kuwatunuku vyeti.
Dream Makers 30 wakiwa na vyeti vya mara baada ya kutunukiwa leo Juni 4, 2022 wakati wa kuhitimisha mafunzo ya wiki mbili.












Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akiwatunuku vyeti Dream Makers 30 mara baada ya kufunzu masomo yao leo Juni 4,2022 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akizungumza wakati akiwatunuku vyeti Dream Makers 30 mara baada ya kufunzu masomo yao leo Juni 4,2022 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akiwa na zawadi mara baada ya kukabidhiwa na Dream Makers 30 jijini Dar es Salaam leo.
Dream Makers 30 wakipamba eneo kwaajili ya kuhitimisha mafunzo jijini Dar es Salaam leo.





Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akiangalia namna ambavyo Dream Makers 30 wamewaremba wenzao ikiwa ni kuhitimisha mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo Juni 4, 2022.









Dream Makers 30 wakiwaremba wenzao ikiwa ni katika kukamilisha mafunzo yao leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad