DKT. STERGOMENA ASHIRIKI UFUNGAJI ZOEZI USHIRIKIANO IMARA NCHINI UGANDA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 11, 2022

DKT. STERGOMENA ASHIRIKI UFUNGAJI ZOEZI USHIRIKIANO IMARA NCHINI UGANDA

 Waziri akiwasili kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa Tanzania walioshiriki Zoezi la Ushirikiano Imara.Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania, Dkt. Stergomena L. Tax, akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mheshimiwa Rebbeca Kadaga, Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu, na Waziri anayehusika na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashari, na Mheshimiwa Jacob Oboth Oboth, Naibu Waziri anayeyusika na masuala ya Ulinzi wa Uganda, pamoja na viongozi mbalimbali wa Afrika Mashariki waliowakilisha nchi zao katika zoezi hilo.

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ameshiriki hafula ya ufungaji wa zoezi la kimedani la ‘Ushirikiano Imara’ lililofanyika Jinja nchini Uganda lililozishirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki isipokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Zoezi hilo ni moja ya jitihada za pamoja za nchi washiriki katika kujiweka tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiulinzi na kiusalama. Zoezi hilo limejikita katika maeneo kadhaa yakiwemo Ulinzi a Amani (Peacekeeping), kukabiliana na majanga (Disaster management), kukabiliana na uharamia (Counter piracy) na kukabiliana na ugaidi (Counter Terrorism) na mengine mengi.

Mara tu baada ya kumalizika kwa hafla hiyo, Mheshimiwa Waziri alipata fursa ya kuongea na Washiriki wa zoezi hilo kutoka Tanzania ambao wanatoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na vyombo vya Usalama kama vile polisi, magereza, uhamiaji, na vyombo vingine vya dola.

Katika kuongea na washiriki hao, Mheshimiwa Dkt. Tax amewapongeza kwa moyo wao wa kujituma na ari kubwa waliyoionesha muda wote wa zoezi na hatimaye kuweza kufanya vizuri. Aidha, amewafikishia salaamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amabye amesema kuwa Serikali inajivunia na kuthamini mchango wao katika kulitumikia Taifa ndani na nje ya nchi, jambo linaloendelea kuiletea nchi yetu sifa kubwa.

Mheshimiwa Waziri pia, amewaasa washiriki hao kuendeleza na moyo wa uzalendo katika kulitetea Taifa letu pamoja na ari waliyoionesha wakati wa zoezi na hata watakaporejea nyumbani Tanzania.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad