HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 14, 2022

DK.SHEIN -AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM

 Na Is-Haka Omar, Zanzibar

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Kikao kilikuwa cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Viongozi mbali mbali walioudhuria kikao hicho ni pamoja Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeil Ali Maulid pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar kilichofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad