HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 15, 2022

CLOUDS YAIOMBA SERIKALI KUINGIZA ELIMU YA USTAWI WA JAMII KATIKA MTAALA ELIMU

Baba na mama Mwita wakisalimiana baada ya kupotezana kwa miaka 22 iliyopita kulia ni Mtangazaji Husna Abdul Da Hu.

Mwita akikumbatiana na mamake Semeni ikiwa ni baada ya kupotezana kwa miaka 22 iliyopita hapo wakiwa wamekutanishwa katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Redio ya Watu Clouds leo Juni 15,2022.
Kijana Boniface Rweyumbiza (33) akilia kwa uchungu mara baada ya kukutana na mama yake mzazi leo Juni 15,2022.

Kijana Anuari aliyeachwa na mamake akiwa na umri  wa miezi miwili akiwa na mamake mzazi baada ya kukutanishwa leo

Kijana Anuari aliyeachwa na mamake akiwa na umri  wa miezi miwili akiwa na mamake mzazi baada ya kukutanishwa leo


Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Kipindi Cha Leo Tena Husna Abdul ambaye pia ni Muongozaji wa kipindi hicho ameiomba Serikali kuingiza mtaala wa elimu ya Ustawi wa jamii ili kuweza kuinusuru jamii na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto kupata haki zao za msingi kutoka kwa baba na mama waliowazaa.

"Elimu ya Ustawi wa Jamii ni muhimu ingefundishwa mashuleni kuanzia darasa la kwanza hadi ngazi ya Elimu ya juu kwa sababu itasaidia wakina mama wanaotelekezwa ama kunyang'anywa watoto wao wakiwa wadogo kutambua haki zao za msingi sambamba na baba kutokwepa kutoa mahitaji ya mtoto husika pindi wawili hao wanapotengana.

Husna alisema hayo leo asubuhi ambapo Kampuni ya Clouds Media Group (MMG) ilipozikutanisha familia tatu tofauti huku kina mama ndiyo walioibuka wakiwatafuta watoto wao ambao kila mmoja alijikuta akigonga mwamba kwa kutafuta familia yake lakini kwa kupitia Kipindi Cha Leo Tena kinachorushwa na Redio ya Watu Clouds wameweza kuwakutanisha.

Michuzi Blog ilishuhudia Anuary Mbaraka (22) akikutanishwa na mama yake mzazi Rehema Said mkaazi wa Masasi aliyemuacha akiwa na miezi miwili huku mtoto huyo akilelewa na Shangazi yake Rehema Said.

Boniface John Rweyumbiza (33) aliyetokea Mkoani Kagera alikutanishwa na mama yake mzazi Happy Kusirie Lema aliyetokea Mkoani Kilimanjaro ambapo ilielezwa kuwa alichukuliwa na marehemu baba yake mzazi akiwa na umri wa miaka mitano tu huku mwanamke mwingine aliyekutanishwa na mtoto wake ni Adam Mwita akitokea Mkoani Mara aliyekutanishwa na mama yake mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Semeni Sultan mkaazi wa Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad