HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 23, 2022

BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA KUENDELEA KUSIMAMIA MICHEZO

 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb)

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma
SERIKALI  imeeleza kuwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania itaendelea kusimamia na kuiratibu sekta ya michezo ya kubahatisha ili iendelee kuchangia katika uchumi wa nchi yetu bila kuleta madhara kwa jamii.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Fatma Hassan Toufiq, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuwanusuru vijana hasa wa kiume wanaoshiriki mchezo wa kamari kwa matarajio ya kupata fedha ya haraka jambo ambalo linaua nguvu kazi ya Taifa.

Mhe. Chande alisema Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania inatekeleza mikakati mbalimbali ili kuhakikisha kwamba jamii inalindwa dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na uwepo wa michezo ya kubahatisha inayosimamiwa na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha SURA 41 pamoja na kanuni zake.

Aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu michezo hiyo ambapo inasisizitizwa kuwa michezo hiyo ni burudani na sio mbadala wa ajira.

“Nawaelekeza waendeshaji wa michezo hii kuzuia ushiriki wa mtu yoyote mwenye umri chini ya miaka 18 na wachezaji wanaobainika kuelekea kwenye uraibu”, aliongeza Mhe. Chande.

Alisema Bodi hiyo pia inafanya ukaguzi kwa kampuni zinazoendesha biashara ya michezo ya kubahatisha ili kuhakikisha zinaendesha michezo hiyo kwa mujibu wa sheria, taratibu na miongozo ya Bodi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad