Mkuu wa Biashara ya kadi NMB, Philbert Casmir akiongea kwenye mkutano huo kwenye hoteli ya Serena Inn mjini Zanzibar leo.
Mkuu
wa wilaya ya Mjini, Mhe. Rashid Simai Msaraka (katikati waliokaa)
katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya NMB baada ya mazungumzo na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena Inn mjini
Zanzibar.
………………………….
Benki ya NMB imefikia makubaliano
na Serikali ya Zanzibar kutunza bustani ya Forodhani visiwani Zanzibar
ikiwa ni moja ya juhudi zake za kuunga mkono azma ya uhifadhi wa
mazingira visiwani humo na ajenda ya uchumi wa bluu.
Mradi huo wa
utunzaji wa bustani ya Forodhani unalenga kuboresha mazingira ya
kitalii na kuakisi vyema sifa maarufu ya eneo hilo, na utawezesha
bustani hiyo kuvutia wageni wengi zaidi kila mwaka huku ukichangia
kuchochea sekta ya utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari
visiwani Zanzibar jana wakati wa kutangaza Mashindano ya Mbio za Boti
Zanzibar yanayodhaminiwa na Benki ya NMB na kutarajiwa kufanyika
Jumamosi hii.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe. Rashid Simai Msaraka
alisema benki hiyo imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo wa serikali ya
Zanzibar na imekuwa mstari wa mbele kusaidia mipango mbalimbali ya
maendeleo visiwani humo.
Alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya
Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi imekuwa
ikiweka kipaumbele cha kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi na
kuzitaka kampuni nyingi kuunga mkono mipango ya maendeleo ya serikali.
“Tumefanya
kazi kwa karibu sana na Benki ya NMB katika miaka ya nyuma na
nimedhihirisha na kutangaza kuwa tayari tumefikia makubaliano nao ya
kuendeleza na kutunza bustani za Forodhani hapa Zanzibar,” Msaraka
alisema.
Alibainisha kuwa pamoja na kuboresha mandhari ya eneo
hilo, mradi huo utaleta manufaa makubwa na kusema, wakandarasi wazawa
watazingatiwa huku akionyesha matumaini kuwa mradi huo utasaidia
kuboresha sura ya Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Kadi
wa NMB, Philbert Casmir wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya
benki hiyo katika kusaidia ushirikishwaji wa fedha na kuongeza kuwa
benki hiyo itaendelea kutoa bidhaa zinazokidhi matakwa ya wateja.
Alisema
mipango ya benki hiyo ni kuendelea kupeleka huduma karibu na wateja
huku akiongeza kuwa benki hiyo ina mpango wa kupeleka huduma kwenye
maeneo ya Wete, Nungwi, Mkoani, Uwanja wa ndege miongoni mwa maeneo
mengine visiwani humo.
Aidha, alisema kama sehemu ya dhamira ya
benki yake kusaidia ushirikishwaji wa kifedha, Jumamosi hii itazindua
Kampeni ya ‘Teleza Kidigitali’ visiwani humo inayotoa huduma za kibenki
bila mafadhaiko na suluhu mbalimbali za kibenki za kielektroniki.
“Baada
ya uzinduzi wenye mafanikio wa kampeni yetu ya ‘Teleza Kidigitali’
katika mikoa mingi nchini Tanzania, sasa ni zamu ya Zanzibar.
Tumejipanga vizuri na kila kitu kipo tayari kwa uzinduzi wa Zanzibar
Jumamosi hii hivyo watu wa Zanzibar wajiandae kupata uzoefu wa kipekee
wa huduma za kibenki za kisasa,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Britam Insurance
wamedhamini mbio za boti za Zanzibar za mwaka huu.
Kampuni hizo
mbili zitatoa zawadi kwa washindi zinazofikia shilingi milioni sita na
laki tano na zitatoa kifurushi cha bima ya ajali kwa washiriki wote kwa
kipindi cha mwaka mmoja.
Friday, June 24, 2022

Home
HABARI
BENKI YA NMB YAKUBALIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR KUSIMAMIA UTUNZAJI WA BUSTANI YA FORODHANI
BENKI YA NMB YAKUBALIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR KUSIMAMIA UTUNZAJI WA BUSTANI YA FORODHANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment