HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 23, 2022

BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2022/2023 NI YA KIZALENDO - KWAGWILWA

 

Na Mashaka Mhando, Dodoma
MBUNGE wa Handeni mjini mkoani Tanga, Reuben Kwagwilwa, amesema bajeti ya serikali ya mwaka 2022/2023 ni ya kizalendo iliyokuwa na mapinduzi makubwa ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza juzi bungeni, mbunge huyo ameipongeza serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuja na bajeti ambayo itamkomboa Mtanzania.

Alisema bajeti hiyo ina mambo makuu mawili muhimu ambayo inaelekeza kubana bajeti katika matumizi na kuimarisha mifumo sheria ya manunuzi.

"Mheshimiwa Naibu Spika nitoe pongezi kwa mheshimiwa Rais mama shupavu, mama mchapa kazi kwa kutuletea bajeti ya kizalendo yenye harufu ya kimapinduzi," alisema mbunge huyo.

Alisema bajeti ya mwaka huu imekuwa tofauti itakayosaidia mambo mbalimbali ya mawndeleo na kutoa mwanga kwa wananchi katika maisha yao ya kila siku.

Alisema mwaka jana serikali ilipanga bajeti ya shilingi trilioni 37.99 na makusanyo ya ndani yalipangwa kukusanya shilingi trilioni 21 lakini hadi kufikia Aprili ilikusanya Shilingi trilioni 17.

"Mwaka huu serikali imepanga bajeti ya shilingi trilioni 41.48 na makusanyo ya ndani itakusanya shilingi trilioni 28.02 kwa maana hiyo TRA inatakiwa ikusanye shilingi trilioni 23.65," alisema.

Hata hivyo, mbunge huyo aliishauri serikali kuboresha kitengo cha kodi ya ushuru wa forodha kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambacho kinahusika na ukusanyaji wa kodi ya forodha katika maeneo matatu ya viwanja vya ndege, bandari na mipakani.

Alisema serikali ikiboresha katika eneo la bandari ambako imewekeza fedha nyingi kwa kuboresha magati namba moja hadi saba katika bandari ya Dar es salaam, kuiwezesha serikali kuongeza mapato.

"Serikali inatakiwa inunue vifaa vya kisasa katika kuhudumia makontena na kifaa hicho ni SSG," alisema.

Pia aliishauri serikali kuhakikisha kwa maboresho waliyoyafanya katika bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara, wasifikirie kuzikodisha ambako hakuwezi kuleta tija kwa Taifa.
Mbunge wa Handeni mjini Reuben Kwagwilwa


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad