HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 2, 2022

AGENDA YABAINI SAMPULI 83 ZA PLASTIKI VYA KEMIKALI VYENYE SUMU

Afisa Program Mkuu wa Shirika hilo, Silvan Mng'anya akitoa taarifa juu ya tafiti nyingi zilizofanywa zimehusisha kemikali sumu ambapo madhara yake ni saratani (Kansa), kuathiri ukuaji wa ubongo kwa watoto, ugumba na utasa pamoja na madhara mengine ya kiafya.

Na Khadija Seif, Michuzi TvSHIRIKA lisilo la kiserikali la Agenda limetoa ripoti ya utafiti mpya uliofanywa hivi karibuni kwa kushirikiana na Mtandao wa Ipen, Arnika na asasi nyengine zilizoshiriki na kubaini kuwa sampuli 83 za plastiki zina viwango vikubwa vya kemikali sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa Program Mkuu wa Shirika hilo, Silvan Mng'anya amesema kuwa tafiti nyingi zilizofanywa zimehusisha kemikali sumu ambapo madhara yake ni saratani (Kansa), kuathiri ukuaji wa ubongo kwa watoto, ugumba na utasa pamoja na madhara mengine ya kiafya.

"kemikali za kuzuia muwako wa moto kwenye bidhaa za plastiki na kemikali sumu zinazozalishwa bila kukusudia hazipaswi kuwepo kwenye midoli ya kuchezea watoto pamoja na kwenye bidhaa za plastiki za nyumbani. " Amesema Silvan.

Hata hivyo, amesema kuwa ripoti ya utafiti mpya uliofanywa katika nchi 11 za Afrika na Uarabuni imebaini kuwa bidhaa 61 zilizozalishwa kwa plastiki zina viwango vikubwa vya kemikali inayopunguza uwezekano wa bidhaa kuwaka moto.

Amesema kuwa, miongoni mwa bidhaa za plastiki kutoka nchini Tanzania zilizojumuishwa katika utafiti huo na kuonesha kuwa na viwango vikubwa vya kemikali za kupunguza muwako wa moto na kemikali nyengine hatarishi zinazodumu kwenye mazingira kwa muda mrefu ni kifaa cha kutunzia kalamu.

Aidha amesema kuwa, Bara la Afrika limegeuzwa kuwa sehemu ya kupeleka taka zenye sumu kinyume Cha sheria kama ilivyoonesha katika utafiti huo ambapo kemikali za sumu zipo katika midoli, vifaa vya jikoni na bidhaa nyengine zinazouzwa kwenye masoko ya nchi za Afrika na Uarabuni.

Amesema kuwa, uchunguzi wa awali wa kutumia mionzi ya X ray umebaini sampuli 83 kuwa na kiwango kikubwa vya kemikali hizo na kuzipeleka kwenye maabara huru kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Aidha amesema vipimo vya maabara vimeonesha kuwa kemikali za BFRs ambazo zimepigwa marufuku kama kemikali sumu zenye kudumu kwenye mazingira kwa muda mrefu chini ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm bado zinapatikana katika bidhaa zinazouzwa katika masoko ya nchi za Afrika na Uarabuni, na kuwa bidhaa nyingi zina viwango vikubwa vya kemikali vya sumu.

Hata hivyo, amesema Agenda,Open, Arnika na asasi nyengine zilizoshiriki katika utafiti huo wamependekeza kuwa taka za kieletroniki na vifaa vya plastiki kutoka kwenye magari yaliokwisha muda wake (ELVs) vyenye viwango vikubwa vya kemikali sumu za kuzuia muwako wa moto vinapaswa kuzuiwa kuingia katika urejelezaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad