Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, mwishoni mwa wiki
alitangazwa kuwa mshindi wa kipengele cha Afisa Mtendaji Mkuu Bora
Africa kwa Mwaka 2022 (Tanzania) katika tuzo zilizoandaliwa na ‘African
Bank 4.0 Summit – CEO Exclusive’ kipengele cha Benki na Uongozi wakati
wa hafla iliyofanyika Ijumaa, Mei 27, 2022 katika hoteli ya Movenpick
jijini Nairobi, Kenya.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Julias Alego -
Mkurugenzi Mtendaji Tasisi ya Mabenki nchini Kenya na kupokelewa na
Mweka Hazina Mkuu wa Benki ya NMB Aziz Chacha.
Akipokea tuzo
hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna,
Chacha alisema, “Ni heshima kubwa sana kwa Ruth Zaipuna kupokea Tuzo ya
“African Banking CEO of the Year 2022 (Tanzania)”
Aidha, baada
ya kupokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Ruth, Chacha alisema kuwa tuzo hiyo
ameitoa kwa wafanyakazi wa NMB kwa kujitolea kwao na nia ya kuendelea
kuwa mstari wa mbele wa vumbuzi, kuzingatia wateja, uthabiti, uaminifu,
na usalama.
"Kwa maneno ya Ruth, natoa tuzo hii maalum kwa moja
ya mtaji wetu mkubwa ambao ni wafanyakazi wa Benki ya NMB, wateja na
wadau mbalimbali ambao bila wao, pengine tusingekuwa hapa
tukisherehekea,” aliongeza.
Alibainisha kuwa benki yake kwa
miaka mingi imekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia shughuli
mbalimbali za kiuchumi katika sekta nyingi ikiwemo Utalii, elimu,
kilimo, miradi ya kimkakati ya muda mrefu na afya.
"Ninatoa tuzo
hii kwa wadau wa Benki ya NMB ambao wamejitolea kikamilifu katika azma
yetu ya kubaki kweli bila kulinganishwa - benki imekuwa mstari wa mbele
kwenye suala zima la ubunifu kwa kuzingatia wateja, uthabiti, uaminifu,
usalama na usalama," aliongeza.
Mnamo Machi 2022, Ruth alitajwa
kuwa miongoni mwa wanawake 74 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika
katika sherehe za wanawake wanaofanya biashara kubwa barani Afrika na
data zilizotumika kutengeneza orodha hiyo ilitolewa kutoka Bloomberg
kulingana na taarifa iliyotolewa na Africa.com.
Thursday, June 2, 2022

Home
BIASHARA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ashinda tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Kibenki Barani Afrika 2022 (Tanzania)
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ashinda tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Kibenki Barani Afrika 2022 (Tanzania)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment