Na Mwandishi Wetu, MOHA, Morogoro.
ZAIDI
ya shilingi Bilioni Tisa (9) zimeokolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi kupitia Idara ya Huduma za Uangalizi kwa kuwasimamia wafungwa
5,000 nje ya magereza ambapo wangetumia zaidi ya shilingi bilioni nne
kwa chakula kama wangebaki magerezani na kupitia shughuli mbalimbali
zinazofanywa bila malipo wanapotumikia kifungo cha nje katika taasisi za
umma nchini.
Akizungumza
katika Mkutano wa Mwaka wa Utendaji wa Viongozi wa Mikoa wa Idara hiyo
ya Huduma za Uangalizi, Mjini Morogoro, leo, Mkurugenzi wa Idara hiyo,
Aloyce Musika alisema idara hiyo imefanikiwa kuokoa fedha hizo kupitia
kazi mbalimbali zinazofanywa na wafungwa wa nje pindi wanapotumikia
vifungo vyao.
Alifafanua
kuwa kwa mwaka wafungwa 5,000 wanaotumikia vifungo vyao vya nje
wanatumia zaidi ya shilingi bilioni nne kwaajili ya chakula kwa kima cha
chini, kupitia kazi wanazo zifanya za usafi na mambo mengine Serikali
ingeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi bilioni tano kama
wangelipwa kima cha shilingi elfu nne kwa mwaka.
Mkurugenzi
Musika aliongeza kuwa, viongozi hao wa mkoa wana jukumu la kuimarisha
ulinzi na usalama katika jamii kwa kuwasimamia wafungwa hao nje ya
magereza, hivyo jukumu lao ni kuhakikisha Wafungwa hao wanapo tumikia
vifungo vyao wanatakiwa kusimamiwa ipasavyo iliwasiweze kutumiwa kwa
kurudia makosa mengine.
“Niwaombe
viongozi waangalizi wa mikoa muwasimamie wafungwa hawa ipasavyo
ilituweze kufanikisha adhima ya Serikali kwa kuaminisha kuwa watu
wanaweza kutumikia vifungo vyao vya nje wakaweza kufanya shughuli
kwaajili ya kuhudumia familia zao na kutumikia adhabu zao na kuiongezea
Serikali fedha”, alisema Musika.
Pia
Mkurugenzi Musika alisema kupitia idara yake wanajipanga kudhibiti
wafungwa wanaorudia makosa baada ya msamaha wa Rais ambao anautoa mujibu
wa sheria.
Aidha,
Afisa Huduma za Uangalizi Mkoa wa Pwani, Subira Majengo alisema
wafungwa wengi wa kifungo cha nje wanatumikia kifungo hicho kikamilifu
na wengi wakimaliza vifungo vyao wanarudi katika jamii wakiwa
wamebadilika na wanaendelea na maisha yao kama kawaida.
Hata
hivyo, aliwaomba wafungwa wanaotikia vifungo vyao nje kuhakikisha
wanakuwa funzo na mfano kwa jamii kuelezea kifungo cha nje kilivyo na
kuhakikisha hawarudii makosa na wanafanya mambo yanayopendeza katika
jamii.
Kwa
upande wake mmoja wa wafungwa wanaotumikia kifungo cha nje, Katika
Halmashauri ya Morogoro, Frolensia Makwaya alisema kifungo hicho
kimemsaidia sana, kwa kuwa ameweza kuendelea na majukumu yake kwa kuwa
anatumikia kifungo chake kuanzia saa kumi na mbili asubuhi na saa nne
asubuhi anaendelea na kazi zake za kawaida.
Alisema
kifungo hicho kimemfanya afanye kazi kwa uchungu ilikuweza kulea mtoto
wake, ameiomba Serikali kuwasaidia na wafungwa wengine kuweza kupata
nafasi ya kuhudumia familia zao kwa kuwa familia nyingi zinateseka.
Mkurugenzi
wa Idara ya Huduma za Uangalizi, Aloyce Musika akizungumza katika
Mkutano wa Mwaka wa Utendaji wa Viongozi wa Mikoa wa Idara hiyo,
uliofanyika katika Hoteli ya Flomi, mjini Morogoro, leo. Amesema zaidi
ya shilingi Bilioni Tisa (9) zimeokolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi kupitia Idara hiyo kwa kuwasimamia wafungwa 5,000 nje ya magereza
ambapo wangetumia zaidi ya shilingi bilioni nne kwa chakula kama
wangebaki magerezani na kupitia shughuli mbalimbali zinazofanywa bila
malipo wanapotumikia kifungo cha nje katika taasisi za umma nchini.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Huduma za Uangalizi (Probesheni), Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Charles Nsanze, akiwasilisha mada kuhusu taarifa ya
utekelezaji wa idara hiyo katika Mkutano wa Mwaka wa Utendaji wa
Viongozi wa Mikoa wa Idara hiyo, uliofanyika katika Hoteli ya Flomi,
mjini Morogoro
Baadhi
ya Viongozi wa Mikoa wa Idara ya Huduma za Uangalizi, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara hiyo (hayupo
pichani) wakati alipokuwa anazungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
wa Mwaka wa Utendaji wa Viongozi hao, unaofanyika katika Hoteli ya
Flomi, mjini Morogoro
Afisa
Huduma za Uangalizi, Mkoa wa Pwani, Subira Majengo akizungumza katika
Mkutano wao wa Mwaka wa Utendaji wa Viongozi wa Mikoa wa Idara hiyo,
uliofanyika katika Hoteli ya Flomi, mjini Morogoro.
Mkurugenzi
wa Idara ya Huduma za Uangalizi, Aloyce Musika (katikati waliokaa),
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, pamoja na Viongozi wa Mikoa wa Idara hiyo, baada
ya kufunguliwa kwa mkutano wa Mwaka wa Utendaji wa Viongozi hao,
unaofanyika katika Hoteli ya Flomi, mjini Morogoro, leo. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment