HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2022

Waziri wa Ulinzi atembelewa na Waziri wa DRC

 

Picha ya Pmaoja

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) Waziri wa Utangamano na Frankafoni, Mheshimiwa Didier Mazenga katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara Mtumba Dodoma.


WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Utangamano na Frankafoni, Mheshimiwa Didier Mazenga katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara Mtumba Dodoma.

Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano wa kindungu na wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili uliodumu kwa miaka miaka mingi tangu nchi hizi zipate uhuru.

Mambo mengine waliyojadiliana ni kuhusu kubadilishana uzoefu wa kuiongoza Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kwa kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatarajia kuchukua uenyekiti wa Jumuiya hiyo ifikapo mwezi Agosti mwaka huu, Jumuiya ambayo Dkt. Stergomena amewahi kuisimamia kwa takribani miaka minane akiwa Katibu Mtendaji tangu mwaka 2013 na kumaliza muda wake rasmi mwezi Agosti mwaka jana.

Aidha, DR Congo kama mwanachama wa Jumuiya hiyo amekuwa wakishirikiana na Tanzania katika maeneo mengi yakiwemo ya ushirikiano kupitia nyanja za ulinzi na usalama. Kwa maana hiyo mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano zaidi kupitia sekta hii.

Kwa kuwa DR Congo ni mwanachama mpya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mawaziri hao pia, wamejadiliana ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana na hatimaye kuweza kuleta maendeleo na Ustawi wa nchi hizi mbili.

Utangamano wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unachagizwa zaidi na utatu, kwa kuwa wote ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi wanachama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad