SERIKALI
imeuelekeza uongozi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inajenga
meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu kuzingatia makubaliano yote yaliyomo
kwenye mkataba wa ujenzi wa meli hiyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Mei 14, 2022
katika kikao kati yake na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo
kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es
salaam.
Katika
Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gas Entec
Tanzania Bw. Kwak ambaye alikiri mapungufu katika utekelezaji wa mradi
huo na aliahidi kuwa kampuni yake itaongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike
kwa wakati na meli hiyo iwezo kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia,
Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelekeza kuwa watalaamu wa Kampuni ya Gas
Entec Tanzania warejeshewe Pasi zao za kusafiria ambazo zilizuiwa na
Serikali kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mwenendo wa ujenzi
wa meli hiyo.
Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika ya Mashariki, Mbarouk Mbarouk na Naibu Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi, Fred Mwakibete.
Wengine
ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli, Philemon
Bagambilana na Kanali Samwel Mahirane ambaye ni Kamishina wa Uhamiaji,
Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kati yake na Balozi wa
Korea Kusini Nchini, Kim Sun Pyo (kulia) kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya
Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2021. Wengine
walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk, Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Makibete, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa
Kazi Tu, Dongmyung Kwak, Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Kanali Samweli Mahirane, Kamishina wa
Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini na Balozi Caesar
Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea
ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo baada ya mazungumzo kati yao kwenye ukumbi
wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14,
2022. Wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk N.
Mbarouk, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Makibete, Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli
ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dongmyung Kwak, Bw. Philemon Bagambilana,
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Kanali Samweli
Mahirane, Kamishina wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini
na Balozi Caesar Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na
Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo kati yao kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2022. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk (kulia kwa Waziri Mkuu) , Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Makibete (kulia) , Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dong Myung Kwak (aliyesimama nyuma katikati), Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (nyuma kushoto) , Kanali Samweli Mahirane, Kamishina wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini (nyuma kulia) na Balozi Caesar Waitara ambale ni Mkurugenzi wa idara ya Asia na Australia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki (kushoto). Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment