Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua Mpango Kabambe wa
Kitaifa wa Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira katika kilele cha Siku ya
Mazingira Duniani Juni 5, 2022 akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip isdor Mpango.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati akitoa tamko la Serikali
kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa kwa vyombo vya
habari leo tarehe 27 Mei, 2022 jijini Dodoma.
Alisema kuwa
Mpango huo umebainisha changamoto za mazingira kuanzia ngazi ya mamlaka
za Serikali za Mitaa, Mikoa pamoja na mifumo-ikolojia mahsusi nchini.
Alifafanua kuwa mpango kabambe huo umetoa mapendekezo ya hatua za
kukabiliana na changamoto husika kuendana na mahitaji ya kila eneo.
Aidha, Waziri Jafo Kwa muktadha huo, Mpango Kabambe wa Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira utakuwa ndio nyenzo muhimu katika kutoa muongozo
wa kuandaa na kutekeleza miradi na programu za kuhifadhi mazingira
nchini,” alisema.
“Mnatambua kwamba nchi yetu inakabiliwa na
changamoto mbalimbali za uharibifu wa Mazingira ikiwemo uharibifu wa
vyanzo vya maji, uharibifu wa Makazi ya wanyamapori na Bioanuai. Hali
hii inasababishwa na matumizi yasiyo endelevu yanayochochewa na
utegemezi mkubwa wa jamii kwenye maliasili,” alisema.
Pia waziri
huyo aliongeza kuwa imebainika takriban kiasi cha hekta 469,420 za
misitu huharibiwa kila mwaka na utupaji holela wa taka pamoja na uwepo
wa athari za mabadiliko ya tabianchi yamekuwa ni changamoto kubwa katika
nchi yetu hali inayoathiri maisha ya viumbe mbalimbali ikiwemo ya
mifumo ikolojia ambapo hadi sasa imeliletea Taifa hasara ya takriban
asilimia tano 5 ya Pato la Taifa.
Alitoa wito kuwa maadhimisho
ya Siku ya Mazingira yaendelee kuwa chachu ya kuongeza kasi ya
uhamasishaji wa jamii kushiriki shughuli za kuhifadhi na kutunza
mazingira nchini.
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
Kitaifa mwaka huu yatafanyika katika hapa Jiji la Dodoma na kaulimbiu ya
kitaifa inayoongoza maadhimisho haya ni ”Tanzania ni moja tu: Tutunze
Mazingira” ambayo inatuhamasisha kwa pamoja kila mmoja katika shughuli
zake za kila siku kutunza mazingira ya nchi yetu ili kuhakikisha nchi
yetu inaendelea kuwa mahali salama pa kuishi kwa vizazi vya sasa na
vizazi vijavyo.
Friday, May 27, 2022

WAZIRI MKUU KUZINDUA MPANGO KABAMBE WA HIFADHI YA MAZINGIRA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment