HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2022

WAUGUZI MKOA WA PWANI KUJENGA CHUO CHA WAUGUZI CHALINZE LENGO KUZALISHA WAUGUZI ZAIDI

 

baadhi ya wauguzi Hospital ya Rufaa Tumbi wakitoa zawadi mama na mtoto mchanga  kwenye wodi ya wazazi hospitalini hapo.

Wauguzi  wakiingia  uwanjani kwa maandamano wakati maadhimisho ya Kilele cha siku ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Tumbi Wilayani Kibaha.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Mkoa wa Pwani (TANNA) Veronica Makange akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Kilele cha siku ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Tumbi Wilayani Kibaha.
Mgeni rasmi mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wauguzi wa Mkoa wa Pwani wakati maadhimisho ya Kilele cha siku ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Tumbi Wilayani Kibaha.
Afisa Michezo Mkoa wa Pwani Grace Bureta (mwenye nguo nyeusi)akishiriki katika  mazoezi ya viungo wakati wa maadhimisho ya Kilele cha siku ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Tumbi Wilayani Kibaha.
Wauguzi na wadau mbalimbali wa afya Mkoani Pwani wakiendelea na mazoezi katika Uwanja uliopo Hospitali ya Rufaa Tumbi.

Na Khadija Kalili
WAUGUZI Mkoa wa Pwani wamejipanga kujenga jengo lao kwa kupitia michango yao ambalo ujenzi huo unaendelea katika Halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika maadhimisho ya Kilele cha siku ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Tumbi Wilayani Kibaha Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Mkoa wa Pwani (TANNA) Veronica Makange alisema lengo la ujenzi wa jengo hilo ni kuzalisha wakunga na wauguzi huku mafunzo yakisimamiwa na wauguzi wenyewe.

Muuguzi huyo aliongeza kwa kusema kuwa kaulimbiu ya mwaka huu inasema muuguzi sauti inayoongoza wekeza kwenye uuguzi heshimu haki kulinda afya kwa wote.

Aidha Katibu wa TANNA Dafroza Mzava alisema kuwa wauguzi wanapitia changamoto nyingi huku akizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na upungufu wa idadi ya wauguzi ndani ya Mkoa wa Pwani, ukosefu wa fedha za mafunzo ya kuniongezea elimu na ujuzi, hawana fedha za manunuzi ya sare zao za kazi, vitendea kazi vichache, kutolewa kauli zisizofaa na zinazowakatisha tamaa katika kazi.

Naye Muuguzi Mkuu wa Mkoa Elizabeth Mlacha alitoa wito kwa wakaazi wa Mkoa wa Pwani kulinda afya zao hasa kwa kuzingatia namna ya aina ya vyakula wanavyokula pamoja na kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi ni afya.

Wakati huohuo Kaimu Msaidizi Idara ya Uchumi Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala ambaye alikua mgeni rasmi huku akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge aliwataasa wauguzi hao kufanya kazi kwa kuzingatia wito na weledi wa kazi ikiwa ni sambamba na kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan licha ya changamoto wanazozipitia huku akiwasisitiza kuwa hakuna kazi ambayo haina changamoto.

Maadhimisho hayo yaliadhimishwa na Wilaya zote tisa zilizopo ndani ya Mkoa wa Pwani ambazo ni Rufiji, Bagamoyo,Mlandizi, Chalinze,Kibiti,Mafia,Rufiji,Kisarawe na wenyeji Kibaha.

Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na utiaji wa huduma za Afya bure zilizotolewa kwa muda wa siku mbili ambazo ni upimaji wa magonjwa ya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi, chanjo ya UVIKO19, kuchangia damu, kupima uzito, kupima sukari na magonjwa mengine mengi.

Pia Wauguzi hao alfajiri waliandamana kwa matembezi ya Kilometa name pamoja na kufanya mazoezi ambapo Ofisa Michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Bureta aliwaongoza huku alisisitiza kwa kusema Michezo ni afya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad