Na Mwandishi Maalum – Chalinze, Pwani 
Wananchi
 437 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari ambapo 
asilimia 60 wamekutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu (Presha) na 
asilimia 20 ya waliokutwa na tatizo hilo tayari walishapata madhara ya 
shinikizo la juu la damu ikiwa ni pamoja na moyo kutokufanya kazi vizuri
 na kutanuka kwa misuli ya damu ya moyo.
Wananchi
 wengine walikutwa na matatizo ya matundu kwenye moyo, mishipa ya damu 
ya moyo kutokukaa katika mpangilio wake, matatizo kwenye vyumba vya moyo
 na mishipa ya damu ya moyo kushindwa kupitisha damu vizuri.
Hayo
 yamesemwa jana na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo
 Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge wakati wa kufanya tathimini ya  
zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari lililofanyika katika 
hospitali ya Halmashauri ya Chalinze iliyopo Msoga wilayani Bagamoyo.
Dkt.
 Kisenge ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha mafunzo na utafiti wa Taasisi
 hiyo alisema wagonjwa 27 walikutwa na matatizo ya moyo yaliyohitaji 
uchunguzi na matibabu ya kibingwa na hivyo kupewa rufaa ya kwenda 
kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
“Katika
 upimaji huu tulifanya upimaji kwa watoto 22 ambapo watatu kati yao 
walikutwa na matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na 
mishipa ya damu ya moyo kutokuwa katika mpangilio wake wa kawaida, 
watoto hawa tumewapa rufaa ya kuja kufanyiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi 
na kutibiwa katika Taasisi yetu”,.
“Zoezi
 la upimaji limeenda vizuri mwitikio ni mkubwa wananchi wamekuja kwa 
wingi na wamefurahia kupata matibabu kutoka kwa wataalamu wetu. Kwa kuwa
 tatizo la shinikizo la juu la damu ni kubwa nawashauri wananchi waepuke
 uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe uliopitiliza na kutokula vyakula 
vyenye mafuta mengi pia wazingatie lishe bora na ufanyaji wa mazoezi kwa
 kufanya hivi wataepuka kupata magonjwa ya moyo”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt.
 Kisenge alisema Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete inaunga mkono jitihada 
za Serikali za kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za matibabu ya 
kibingwa kwa kuwafuata wananchi mahali walipo kwa ajili ya kutoa huduma 
za upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari bila malipo yoyote yale kwa 
kufanya hivi wananchi wengi wataweza kufikiwa na huduma za matibabu ya 
kibingwa ya magonjwa hayo kwa haraka zaidi.
Naye
 Mganga mkuu wa Halmashauri ya Chalinze Dkt. Allen Mlekwa  aliwashukuru 
wataalamu waliotoa huduma za upimaji na matibabu kwa wananchi na kusema 
upimaji huo ulihusisha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI 
pamoja na wenzao wa Hospitali ya Msoga.
Dkt.
 Mlekwa alisema waliokutwa na matatizo ya  moyo wengine walikuwa na 
kliniki katika hospitali mbalimbali na walikuwa wanatumia dawa lakini 
waliacha kutokana na sababu mbalimbali na baada ya kufanyiwa vipimo vya 
moyo wamekutwa mioyo yao imetanuka na wengine wamekutwa na ugonjwa sugu 
wa kisukari. Baadhi yao hawakuwa wanafahamu kabisa kuwa na tatizo la 
moyo na hivyo waliwaanzishia dawa za kutumia.
“Kuwepo
 kwa zoezi hili la upimaji kumetufanya tufahamu kunatatizo kubwa la watu
 wenye matatizo ya moyo na kisukari  hivyo basi nasi tumejipanga 
kuboresha kliniki yetu ya moyo na kisukari iliyopo katika Hospitali ya 
Msoga kwa siku ya alhamisi ili wagonjwa waliokuwa wanakwenda kutibiwa 
Hospitali za Tumbi, Amana, Mwananyamala na Muhimbili waje kutibiwa 
hapa”,.
“Kwa
 kuwa tuna mashine za kupima vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya
 kazi (Echocardiography – ECHO) na kuchunguza mfumo wa umeme wa moyo 
(Electrocardiography - ECG) tutawafanyia wagonjwa wenye shida ya moyo 
vipimo hivi hapa hapa na kama tutawakuta na matatizo makubwa tutawarufaa
 kwenda kutibiwa katika Hospitali kubwa zaidi”,.
“Wananchi
 wengine wametoka kilomita zaidi ya 100 karibu kabisa  na Tanga na 
Mvumero wamekuja hapa kwa ajili ya kufuata huduma hii ya upimaji, 
tutajipanga ili tuweze kufanya mobile kliniki za kwenda kutoa huduma za 
upimaji katika vituo vya afya vya Msata, Kibindu, Lugoba na Miono kwa 
kufanya hivi wananchi wengi watafikiwa na huduma za matibabu ya moyo na 
kisukari”, alisema Dkt. Mlekwa.
Kwa
 upande wa wananchi waliopata huduma hiyo walishukuru kwa huduma ya 
uchunguzi na matibabu ya bila malipo  waliyoipata na kusema 
imewapunguzia gharama ya kusafiri na kuwafuata wataalamu Dar es Salaam 
pamoja na kulipia matibabu hayo.
Fredrin
 Ikumbera mkazi wa Lugoba alisema alipima vipimo na kukutwa moyo uko 
sawa lakini amekutwa na shida ya presha amepewada dawa za kutumia pamoja
 na  ushauri wa lishe bora na kuambiwa apunguze matumizi ya vyakula vya 
wanga pamoja kupunguza kunywa pombe kwani ni hatari kwa afya ya moyo 
wake.
“Nilikuwa
 ninawasiwasi kuhusu moyo wangu kwani mazingira niliyokuwa naishi 
hayakuwa salama. Ninawasihi wananchi wenzangu kutumia  nafasi za upimaji
 pindi zinapotokea kwa kwenda kupima afya zao pia kwa upande wa Serikali
 iendelee kuhakikisha wananchi walioko vijijini wanapata huduma za 
matibabu ya kibingwa kwani kutokana na mazingira yao ni vigumu kufikiwa 
na huduma hizi”, alisema Ikumbera.
Afisa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aliston Jovin 
akiwagawia vipeperushi vinavyoelezea huduma za matibabu zinazotolewa na 
JKCI wananchi waliofika katika Hospitali ya Halmashauri ya Chalinze 
iliyopo Msoga kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo 
uliofanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI katika Halmashauri hiyo 
iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.Afisa
 Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rahabu Tamba 
akimpima urefu na uzito mwananchi aliyefika katika Hospitali ya 
Halmshauri ya Chalinze iliyopo Msoga wilayani Bagamoyo kwa ajili ya 
kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo uliokua ukifanywa na wataalam wa 
moyo kutoka JKCI kwa wananchi wa Chalinze.  Daktari
 kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Ng’ondya 
akimuelezea mwananchi umuhimu wa kutumia dawa za shinikizo la damu 
wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo la damu 
uliofanywa na wataalam wa moyo kutoka taasisi hiyo kwa wananchi wa 
Chalinze kwa siku mbili na kumalizika jana katika Hospitali ya 
Halmashauri ya Chalinze iliyopo msoga Wilayani Bagamoyo.
Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akisoma majibu ya vipimo vilivyofanywa na mwananchi wa Chalinze baada ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa upimaji uliyofanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI kwa wananchi wa Halmashauri ya Chalinze iliyopo wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Tafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kiwetwe (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima mwananchi wa Halmashauri ya Chalinze kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo-Cardiograph) wakati wa upimaji uliofanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI kwa wananchi hao siku mbili katika Hospitali ya halmashauri hiyo iliyopo Msoga wilayani Bagamoyo.Wataalam wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa upimaji maalum uliofanyika kwa siku mbili kwa wananchi wa Chalinze kuchunguza magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo la damu katika Hospitali ya Halmashauri ya Chalinze iliyopo msoga wilayani Bagamoyo. Picha na JKCI
Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akisoma majibu ya vipimo vilivyofanywa na mwananchi wa Chalinze baada ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa upimaji uliyofanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI kwa wananchi wa Halmashauri ya Chalinze iliyopo wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na Tafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kiwetwe (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima mwananchi wa Halmashauri ya Chalinze kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo-Cardiograph) wakati wa upimaji uliofanywa na wataalam wa moyo kutoka JKCI kwa wananchi hao siku mbili katika Hospitali ya halmashauri hiyo iliyopo Msoga wilayani Bagamoyo.Wataalam wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa upimaji maalum uliofanyika kwa siku mbili kwa wananchi wa Chalinze kuchunguza magonjwa ya moyo, kisukari na shinikizo la damu katika Hospitali ya Halmashauri ya Chalinze iliyopo msoga wilayani Bagamoyo. Picha na JKCI







No comments:
Post a Comment