HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 12, 2022

VIJIJI 100 KUFAIDIKA NA MRADI MPYA WA MBOLEA OCP MKOA WA RUVUMA

 Na.Khadija Seif, Michuzi TV

KAMPUNI kinara katika uzalishaji wa mbolea ulimwenguni PCP, imezindua rasmi mradi wa “OCP School Lab” kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Ruvuma mradi unaolenga kutoa elimu kwa wakulima juu ya afya ya udongo, mbinu sahihi kwa mazao husika.

Uzinduzi wa mradi huu umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya “Heritage Cottage” uliopo mjini Songea Mei 12, 2022 na kuhudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na wilaya zake na walijionea teknolojia juu ya ukemia wa udongo na mapendekezo ya mbolea kutokana na aina ya udongo husika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Ndugu Joseph Mkirikiti, Mkuu wa wilaya ya Kalambo Ndugu Kalolius Misugwi amesema, sekta ya kilimo imeajiri namba asilimia 65% ya watanzania wote na imelihakikishia taifa upatikanaji wa chakula kwa asilimia 100% pamoja na malighafi za viwandani, lakini bado idadi hiyo ya watanzania wanaojishughulisha kilimo haipo katika uwiano sawa na idadi ya watanzania wote na hii ni kwa sababu ya tija ndogo inayotokana na uzalishaji mazao.

"Hivyo mpango huu utasaidia kuongeza na tija na bila shaka kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo Huku lengo likiwa ni kuogeza tija kwenye kilimo, ubora na ustawi na mazao na niwapongeze sana kampuni ya OCP Afrika kwa kuandaa mradi huu ili kusaidia kutathimini rutuba ya udongo katika ngazi yamkulima kwa vijiji 400 katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa na Morogoro na kwamba kazi hiyo itafanyika bila malipo yoyote”.

Kwa upande wakeMkurugenzi mkuu wa kampuni ya OCP Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema, "OCP Tanzania ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo kwa zaidi ya vijiji 100 ndani ya mkoa wa Ruvuma.

Msolla amefafanua zaidi Lengo ni kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote kwa wakulima hao.

"Majibu yatatolewa kwao na kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) tutatoa ushauri wa kitaalamu juu ya nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo wa kijiji husika kwa matokeo bora ya shughuli za kilimo Katika kila kijiji zaidi ya wakulima 100 ".

Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo kwa mwaka 2022 unatarajiwa kuendeshwa katika vijiji 600 na kuwafikia wakulima wapatao 60,000 kufikia mwisho wa mwaka 2022. Mradi huu pia unatarajiwa kutoa tathmini ya udongo na mapendekezo ya matumizi ya mbolea kwa wakulima wapatao 12,000 watakao wakilisha wakulima wenzao kutoka mashamba mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

"Ni jambo lenye ulazima, kwamba wakulima wetu wawe rafiki wa teknolojia za kisasa zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji wao, na hivyo kuondokana na umasikini. Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo ni jambo la kipekee sana na hivyo tunahamamisha wakulima wote wawe sehemu ya mradi huu". Aliongeza Dkt. Msolla.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uzinduzi wa mradi huu umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya “Heritage Cottage” uliopo mjini Songea Mei 12, 2022 na kuhudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na wilaya zake akiwemo Mkuu wa wilaya ya Kalambo Kalolius Misugwi pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya kinara Kwa uzalishaji wa mbolea duniani ocp.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Kalolius Misugwi akisikiliza kwa makini Malengo ya kampuni ya uzalishaji wa mbolea duniani ocp na kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad