HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 7, 2022

VIJANA WATAKA UWAZI KUHUSU AFYA YA UZAZI

 

VIJANA wamesema kuwa wanataka uwazi kuhusu afya ya uzazi kuanzia kwenye ngazi ya familia hadi Taifa ili kuweza kukwepa madhara yanayoweza kujitokeza kama vile maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Wakizungumza katika kongamono la afya ya uzazi kwa vijana wamesema pia taarifa sahihi ni muhimu kwa vijana ili kufanya maamuzi sahihi kuhusu mahusiano.

Innocent Grant ni miongoni mwa vijana hao alisema umuhimu wa uwazi na taarifa sahihi inasaidia vijana kuwepa mimba za utotoni ,virusi vya Ukimwi ,ndoa za utoto na magonjwa ya zinaa.

“Tunahitaji kubadilisha vijana kifikra kuhusu mahusiano na pia waadishi wanajukumu kubwa katika hili.”alieleza.

Alibainisha kuwa mpango huo unaambatana na mabadiliko ya sera rafiki kuhusu masuala ya uzazi na upatikanaji wa huduma rafiki kwa vijana wa maeneo ya mjini na vijijini.

Innocent alisema madhara ya ngono kwa vijana yanazuilika endapo watapata elimu mapema.

“Kingine jamii iache kutoa elimu ambayo sio sahihi au mafumbo kwa kuwaambia mapenzi ni mabaya ,wanatakiwa kuwaeleza ukweli na kuwaelekeza namna bora ya mahusiano,”alifafanua Innocent.

Naye Lilian Matthew, Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alisema madhara ya ukatili wa kijinsia ni kupoteza maisha na kilema cha kudumu.

“Ukatili wa kijinsia hauvumiliki hivyo serikali itoe semina mbalimbali ili vijana wapate elimu na jamii isikubali kuvumilia wa kijinsia na kingono,”alisisitiza Lilian.

Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa Vyuo na Shule (YUNATZ) Abdul Shaban alisema elimu kuhusu afya ya uzazi inatakiwa kuanza kutolewa katika ngazi za shule ya msingi na ngazi ya familia .

“Kuna umri ukifika mtoto anatakiwa kupata elimu kuhusu magonjwa ya ngono na sio kweli kuwa ukiwaambia ukweli unawaharibu ila unamsaidia.”alisema Abdul.

Naibu mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) Dk Wilferd Ochan alisema michezo na burudani inanafasi kubwa sana katika kuhamasisha vijana kupata elimu kuhusu afya ya uzazi.

“Ni muda sasa vijana kupata elimu sahihi kuhusu afya ya uzazi kupitia njia mbalimbali hasa zile vitu ambavyo wanavipenda kama vile michezo na muziki .

Alisema hatua hiyo itasaidia vijana wengi kupata elimu kwa maeneo yote na pia kuweza kupinga ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad