Na Mwandishi Maalumu -Acrra-Ghana
Ubalozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Nigeria, Wenye Uwakilishi
Sambamba nchini Ghana, umefanya Kongamano la Utalii, Uwekezaji na
Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and Trade Forum (TG-TITF),
Mei 28, 2022, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Nigeria, wenye Uwakilishi Sambamba nchini Ghana, umefanya Forum ya
Utalii, Uwekezaji na Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and
Trade Forum (TG-TITF), Jijini Accra, Ghana.
Jukwaa
hilo lilikusudi kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania Bara na
Zanzibar, fursa na vivutio vya uwekezaji pamoja fursa za biashara.
Jukwaa hilo liimefunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, ambapo pia limehudhuriwa
na wadau wa sekta hizo kama vile Jumuiya za Wafanyabiashara,
Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za Ghana, Makampuni ya Utalii,
Wafanyabiashara na Wawekezamitaji.
Katika
kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, na Madini ya Ghana, Clement Osei-Amoako.
Aidha,
Taasisi za Jamhuri ya Muungano, hususani TTB, TIC, ZIPA, EPZA,
TanTRADE, Jumuiya za Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za
Tanzania Bara na Zanzibar, zilishiriki na kuelezea kwa undani fursa,
miundo, majukumu na nafasi zake katika kukuza Biashara, Utalii na
Uwekezaji nchini Tanzania.
Pamoja
na mambo Mengine, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria anbaye pia
anawakilisha nchi ya Ghana Dk. Benson Bana, alieleza kuwa Jukwaa hilo
linakusudia kuleta taasisi, jumuiya za wafanyabiashara, wawekezaji wa
Tanzania na Ghana kuona namna ya kushirikiana na kukuza mahusiano ya
uwili baina ya nchi hizi, ambazo uhusiano wake ulianzatangu kipindi cha
waasisi wa mataifa haya, Mwl. Julius Nyerere na Mhe. Kwame Nkrumah,
Marais na Baba wa Mataifa ya Tanzania na Ghana mtawalia.
Aidha,
juhudi hizi ni kuunga mkono Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika
kukuza sekta ya Utalii hasa kupitia Filamu ya “The Tanzania Royal
Tour”.
Kwa
Upande wake Balozi Mstaafu wa Ghana nchini Ufaransa, Genevieve Delali
Tsegah, Balozi Mstaafu wa Jamhuri ya Ghana nchini Ufaransa, alipongeza
hatua hiyo na kusema kuwa itakwenda kufungua milango ya utalii na
uwekezaji nchini Tanzania kutokana na kazi kubwa inayofanywa na viongozi
wake
Naye Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kwaku Group, Dk. Ken Kwaku, ambaye pia ni Balozi wa Heshima nchini Tanzania,
Mkurugenzi
na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Utalii ya Ghana aliyewakilishwa na
Alfred Asumadu Naibu Mkurugenzi wa Masoko pamoja na Bi. Alisa
Osei-Asamoah, Rais wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii Ghana (Tour
Operators Union of Ghana), Dkt. Sarah Marjie, Mhadhili Mwandamizi, Chuo
Kikuu Cha Ghana Lego, na Mratibu wa masomo ya Lugha ya Kiswahili
waliwasilisha salaam na kuchangia katika Mada mbalimbali.
Aidha,
Jukwaa hilo lilihudhuriwa na baadhi ya Watanzania waishio nchini Ghana.
Wanafunzi wa Lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Ghana Legon
walishiriki na kuhudumia jukwaa hilo ili kuwa karibu na Tanzania ambako
Lugha ya Kiswahili ilizaliwa.
No comments:
Post a Comment