HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 14, 2022

TUNAMATEGEMEO MAKUBWA KWENU- DEJEMBI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akitunuku Cheti mmoja ya Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi leo Mei 13, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) wakiwa na vyeti vyao mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao katika Ukumbi wa Mlimani City jiji Dar Es Salaam, Mei 13, 2022.


Baadhi ya wahitimu wakisikiliza viongozi mbalimbali wakati wa Mahafali yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam leo Mei 13, 2022.

Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi katika Taasisi ya Uongozi wakiingia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam leo Mei, 13 Wakati wa mahafali ya tano ya wahitimu wa Diploma ya uongozi na ngazi ya cheti cha Uongozi.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
MATEGEMEO yetu kwenu nimakubwa mno, mafunzo yameisha sasa mnatakiwa kuonesha kile mlichojifunza kwa vitendo, tunataka kuona uongozi wa kimkakati tunataka kuona mkisimamia vizuri rasilimali watu na rasilimali fedha, tunataka kuona mboresho makubwa katika nyanja ya mawasiliano na mahusiano katika baina yenu nyinyi kama watumishi wa umma lakini pia mawasiliano na mahusiano baina yenu na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ndani na nje ya nchi yetu."

Hayo ameyasema Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius  Ndejembi wakati wa mahafali ya tano ya Mafunzo ya Stashahada ya Uzamili ya Uongozi pamoja na mafunzo ya uongozi kwa njia ya mtandao kwa ngazi ya cheti yanayotolewa na Tasisi ya Uongozi ikishirikiana na chuo cha Aalto EE cha Nchini Finland Mlimani City jijini Dar Es Salaam Mei 13, 2022.

Amesema Nchi yetu imejaliwa rasilimali mbalimbali, Madini, Mito, Bahari, mimea n.k ili rasilimali hizi ziwe na manufaa kwa taifa lazima kuwe na rasilimali watu wenye weredi wa kutosha hivyo mafunzo waliyo yapata ni sehemu ya kuwajengea uwezo kwaajili ya kusimamia rasilimali zetu kikamilifu kwa mstakabali wa taifa.

"Kiongozi mzuri ni yule anayewajibika na kutekeleza majukumu yake bila kushurutishwa....." Amesema Ndejembi

Amesema mategemo ni kuona utumishi bora wenye msingi imara na thabiti kiuongozi na kiutendaji mara baada ya kurejea sehemu za kazi wahitimu hao wa mahafali ya tano.

Licha ya hayo amewakaribisha rasmi washiriki wa awamu ya sita katika mafunzo ya uongozi, " Matumaini yangu washiriki wapya mtafuata nyayo za wenzenu na ikiwezekana mfanye vizuri zaidi ili muache alama, nawasihi mtoe ushirikiano mzuri kwa waendeshaji wa mafunzo hayo..." Amewaasa ndejembi

Amewaomba Taasisi ya Uongozi kuandika tawasifu ya Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na  Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Magufuli pia amewapongeza kwa kwa kuandika tawasifu za viongozi wa awamu ya pili na tatu.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Kiongozi Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said amewaasa viongozi kutokuwa wabinafsi pale zinapotokea fursa mbalimbali katika jamii.

"Wengine wanakuwa wanajali  wa Kwao na Jamaa zao.. wengine husema kutesa kwa zamu kwakuwa mwezao yupo juu pale..., hivi hatakiwi kwa kiongozi..." Amesema Injinia Zena

Amesema viongozi wengine wanafikilia kuwa Uongozi ni kama ajira ya kawaida na kupata mshahara wake, lakini dhima kubwa ya Uongozi ni kuonesha njia kwa wengine mfano mahali popote penye  kiongozi panatakiwa kujulikana kama yupo.

Amesema kiongozi anatakiwa kuwa kuwatia moyo wengine walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao, sio kuwavunja moyo au kuwa na kauli za kudharau na kukatisha tamaa katika kazi na jitihada wanazojaribu kuonesha mahali pa kazi. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) Dkt. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo kwa viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam na kuzisaidia taasisi mbalimbali pamoja  na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) ilianzishwa Julai, 2010 kwa malengo ya  kuwa na kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza viongozi barani Afrika kwa kuanzia nchini Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.

Katika Mahafali ya tano ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) jumla ya wahitimu 41 wamefunzu Stashahada ya Umahili ya mafunzo ya Uongozi na mafunzo kwa njia ya mtandao kwa ngazi ya  Cheti cha Uongozi 76 wamefunzu na kutunukiwa vyeti vyao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad