HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2022

RAIS SAMIA MGENI RASMI TUZO ZA WANDISHI WA HABARI MEI 28, 2022

 Mmoja ya jopo la majaji walio pitia kazi 598 za waandishi wa habari akizungumzia changamoto walizozipata wakati wa kupitia kazi za waandishi wa habari na kupata kazi 60 zilizobora zaidi kwaajili ya kuwatunukia tuzo waandishi wa kazi hizo kwa mwaka 2021. kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi EJAT, 2021, Kajubi Mukajanga.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi EJAT, 2021, Kajubi Mukajanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 19 2021 wakati wa kutambuliza tuzo za umahili katika uandishi wa habari kwa mwaka 2021.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwamgeni rasmi katika utoaji za umahili wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT), 2021 na ndiye atakaye mkabidhi Tuzo mshindi wa jumla pamoja na mshindi wa Tuzo ya Maisha ya Mafanikio Katika Uandishi wa Habari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Mei 19 2021 , Mwenyekiti wa Kamati ya Maadalizi EJAT, 2021, Kajubi Mukajanga amesema kuwa tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mei 28, 2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa idadi ya wateule wa EJAT 2021 kwa upande wa wanawake ni 28 ambayo ni sawa na asiliamia 47, ikiwa ni ongezeko la asilimia tatu ukilinganisha tuzo zilizopita ambapo wanawake walikuwa ni 26 sawa na asilimia 44 walioingia kwenye kwenye hatua hii kwa mwaka jana. Na wateule wanaume ni 32 sawa na asilimia 53.

Amesema kuwa jopo la Majaji lilikaa na kupitia kazi 598 za waandishi zilizokuwa katika makundi 20 yanayoshindaniwa katika tuzo za umahili wa Uandishi wa habari Tanzania (EJAT) 2021 na kufanikiwa kuteua waandishi 60 ambao kazi zao zimeonekana kuwa bora zaidi.

Kati ya wateule hao 60 tisa wanaandikia Runinga, 12 vyombo vya Mtandaoni, wanne redio na 31 wanaandikia Magazeti.

Kati ya wateule 28 wanawake 18 wanatoka katika magazeti, runinga wametoka watatu, radio wawili na vyombo vya habari vya mtandaoni watano, Kwa upande wa waandishi wa habari wanaume, magazeti wametoka 12, runinga waandishi sita, radio wateule sita na vyombo vya habari vya mtandaoni wateule saba." Amesema Mukajanga.

Amesema Kwa mujibu wa majaji wa EJAT 2021, kazi za mwaka huu, zimeonyesha kuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na mwaka jana. Hiyo ni pamoja na kiwango cha waandishi wa habari wa vyombo vya mtandaoni kuonyesha kukomaa zaidi katika kazi zao na mwamko wa ushiriki katika Tuzo hizo.

Makundi yanayoshindaniwa katika Tuzo za EJAT 2021 ni Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi, Tuzo za Uandishi wa Habari za Data, Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu, Tuzo za Uandishi wa Habari za Utawala Bora na Uwajibikaji.

Mpiga Picha Bora- Magazeti, Mpiga Picha Bora- Runinga, Mchora Katuni Bora,Tuzo ya uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini, Tuzo za Uandishi wa Habari za Walemavu, Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya na Tuzo ya Uandishi wa Sayansi na Teknolojia.

Tuzo hizo zimefadhiliwa na Wajibu Institute, Natural Resources Governance Institute NRGI, washiriki, Kituo cha Msaada wa Kisheria, na Haki za Binadamu (LHRC), Busota Inn, Serena hotel Dar es Salaam, Coca Cola, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Azam Media, Twaweza na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Hii itakuwa ni mara ya 13 kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi katika mwaka 2021.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad