HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2022

NHC YAPONGEZWA KWA MAONO NA KAZI NZURI LINAZOFANYA

Waziri wa Ardhi, Nymba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akifungua semina ya Wabunge iliyotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa leo jijini Dodoma. Walioketi wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Allan Kijazi, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii, Ally Makoa na mwisho kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Rihiwani Kikwete. Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Nyumba la Taifa limepongezwa kwa kazi nzuri linazozifanya na pia kuwa na maono makubwa kuhusu mwelekeo wa nchi na wa wananchi kwa ujumla kuhusiana na masuala ya makazi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakichangia mawazo kwenye semina kwa wabunge juu ya uelekeo wa Shirika, Wabunge hao walilipongeza Shirika kwa majukumu linayoyatekeleza kwa sasa.

Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu ameamelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kazi nzuri lakini pia kwa kuwa na maono makubwa na yenye msingi wa kuboresha makazi ya binadamu ngawa pia akatoa changamoto kuhusu matengenezo ya nyumba hizo.

Naye Mheshimiwa Hawa Mwaifunga Mbunge wa Viti Maalumu alimpongeza Mkurugenzi Mkuu kwa kuteuliwa tena na kuwa ana imani kuwa miradi iliyokwama katika jiji la Dar es Salaam itakwamuliwa na kuendeleza mingine mipya ambayo itawapa faida kubwa ya makazi watanzania.

Mheshimiwa Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo amesema kuwa “Nawapongeza sana kwa maono makubwa na mazuri mliyo nayo, nilikuwa sijui kama lile jengo la Makao Makuu ya CRDB ni idea yenu . Msitizame mijini tu mtujengee na siii kwetu kule Namtumbo na pia kule Nyassa, tufikireni na sisi tumekwishawatengeeni maeneo bure.”

Akifungua Semina hiyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Dk Angeline Mabula imelielekeza Shirika la Nyumba la Taifa kuangalia namna ya kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika maeneo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na Halmashauri za Miji na Wilaya nchini.

Amelitaka Shirika pia kutumia fursa ya mikopo ya nyumba kufanya uendeleezaji mkubwa wa nyumba za makazi kuliko kubakia na upangishaji wa nyumba chache zilizorithiwa.

Pia amelitaka Shirika Kutumia rasilimali nyumba walizo nazo katika mikoa mbalimbali kujiendesha kibiashara na kuweza kupata mikopo ya kujenga nyumba nyingi ili kukidhi mahitaji ya nyumba nchini na kushirikiana na wawekezaji binafsi ili kufanya uwekezaji mkubwa wa majengo ya biashara na makazi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa akizungumza katika Semina hiyo amesema kuwa Shirika limeboresha Mpango Mkakati wa Shirika ili uweze kukidhi matarajio ya Serikali na nchi kwa ujumla.

Pia amesema Shirika limeboresha muundo wa utendaji wake ili uweze kubeba majukumu yaliyoainishwa kwenye Mpango Mkakati na pia limeboresha sera mbalimbali ikiwemo sera ya ubia ambayo ni vizuri Waheshimiwa Wabunge mkafahamu.

Amesema kwamba kwa sasa Shirika lipo katika mkakati wa kukamilisha miradi mitatu ya nyumba iliyokwama kwa miaka takribani minne katika Jiji la Dar es Salaamya Kawe 711, Morocco Square na GPR pia kujenga nyumba mpya 500 katika eneo la Kawe, kuongeza nyumba za makazi na kipaumbele katika jiji la Dodoma, kukamilisha majengo ya kudumu ya Wizara nane za Serikali katika Mji wa Mtumba.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akitoa Semina kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu akichangia kwenye semina hiyo.
Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika ukumbi wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mijadala katika semina ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad