HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2022

MWAMUZI WA KIKE KUTOKA AFRIKA ATEULIWA KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA

 Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MWAMUZI wa kati, Salima Mukansanga kutoka nchini Rwanda amekuwa mmoja kati ya Waamuzi Sita wa Kike walioteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuchezesha Michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18, 2022.

Mtandao wa Mozzartsport wa Kenya umeripoti kuwa Salima na wenzake, Stephanie Frappart (France) na Yoshimi Yamashita (Japan) wametangazwa kuingia kwenye orodha ya Waamuzi ambao watachezesha Michuano hiyo mikubwa duniani, huku Waamuzi wengine watatu wakiwa kwenye orodha ya Waamuzi Wasaidizi ambao ni Neuza Back (Brazil), Karen Díaz Medina (Mexico) na Kathryn Nesbitt (USA).

Wanawake hao wanatengeneza historia mpya katika Soka la ulimwengu katika kipindi cha miaka 92 iliyopita. Mwezi Januari mwaka huu

Mwanamama Mukansanga aliandika historia nyingine baada ya kuwa kwenye jopo la Waamuzi walichezesha Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON)

Kwa ujumla, Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka (FIFA) imeteua idadi ya Waamuzi 36, Waamuzi Wasaidizi 69 na Waamuzi 24 wa VAR kutoka Mashirikisho Sita yenye ubora na kukidhi vigezo vya FIFA katika miaka ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad