HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 29, 2022

MARIE STOPES TANZANIA, FLAVIANA MATATA FOUNDATION KUSHEREKEA SIKU YA HEDHI DUNIANI KWA KUTOA ELIMU KWA WANAFUNZI MWANZA

 






WAKATI  leo ikiwa ni siku ya maadhimisho ya Hedhi Duniani ambayo huadhimishwa kila Mwaka tarehe 28 Mwezi Mei,Shirika la Marie stoipes Tanzania kushirikiana na Flaviana Matata Foundation wametoa Elimu ya masuala ya hedhi salama kwa wasichana na wavulana 987 katika shule ya Sekondari ya Bukandwe ilioko wilaya ya Magu Mkoa wa Mwaza.

Kupitia taarifa iliyotolewa na mashirika hayo kwa vyombo vya Habari nchini katika siku hiyo iliyobeba kauli mbiu ya Hedhi iwe kama ni moja ya Maisha ya Kawaida kwa msichana na Mwanamke inasema lengo siku hiyo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali ili kuwaongezea uelewa kuhusu maswala ya hedhi kwa msichana,kuhamaisha msichana kupata maji safi na taulo hasa wale walio katika mazingira ya hali ya chini ili wanapoingia katika siku zao za hedhi aweze kujisitiri na kuendelea na taratibu zingine kama kuhudhuria masomo na shughuli nyingine.

“Hii ina maana tuwe na dunia ambayo hakuna mtu ataachwa nyuma au atashindwa kufikia malengo yake au kufanya shughuli zake za kila siku kwa sababu tu anaingia kwenye siku za hedhi.”inaeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo,mara baada ya mafunzo mashirika hayo yaliwashika mkono wanafunzi hao kwa kutoa Zawadi mbalimbali ikiwemo taulo za kike kwa wasichana ili kuhakikisha suala la hedhi lisiwe kikwazo kwa mtoto wa kike kwa sababu wapo baadhi yao wanakosa raha pindi wanapokaribia mzunguko wao.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa zipo baadhi ya changamoto zinazomkwamisha mtoto wa kike ikiwemo mila potofu kwa sababu mwanamke au msichana aliye kwenye hedhi hapaswi kugusa maji, kupika, kushiriki sherehe za kidini au hata za kijami hivyp fikra hizo potofu husababisha ubaguzi na kuendeleza Imani potofu juu ya wanawake wanapokuwa katika siku zao za hedhi kuwa ni wachafu.

Kutojihusisha katika shughuli mbalimbali za jamii kutokana na kukosekana kwa nyenzo ambazo zitamsaidia mtoto wa kike katika kipindi aonapo hedhi basi mara nyingi watoto hawa hujitenga katika shughuli mbalimbali kama vile shule ile.

Pia,kukosa fursa kama mwanamke atakuwa wa kukaa tu nyumbani kipindi akiwa kwenye siku zake sababu tu amekosa vitu vya kumsaidia kupata hedhi salama basi ni wazi kuwa atakuwa anakosa fursa nyingi sana zinazoweza kujitokeza katika jamii yake kipindi yeye akiwa katika siku zake za hedhi.

Katika kuadhimisha siku hii tunatoa wito kwa mashirika binafsi,serikali na walimu kusisitiza utolewaji wa Elimu ya masuala ya hedhi kwa Vijana wa kiume na wa kike kwa sababu kwa kufanya hivyo itamsaidia msichana kutambua mabadiliko ya mwili na kukabiliana nayo pamoja na kufahamu namna ya kujisitiri kipindi anachoingia kwenye hedhi, na kwa mvulana kuelewa mabadiliko hayo kama mshiriki mwenza ili kuondoa unyanyapaa pale msichana anapokuwa kwenye hedhi.

Kwa mashirika ya afya mashirika ya maendeleo na taasisi mbalimbali kuzisaidia jamii kwa namna mbalimbali kuhakikisha wasichana hasa walio mashuleni wanakuwa na mazingira rafiki ili wanapoingia kwenye siku zao za hedhi wasikose mahitaji yao muhimu yatakayowasababisha kushindwa kushiriki kwenye masomo na masuala mengine ya jamii kutokana na hedhi .

Pia,kuliangalia swala la utaratibu wa bei za taulo za kike, upatikanaji wa maji safi na salama katika shule , kusaidia maeneo yenye uhitaji ili wasichana waweze kupata taulo za kujisitiri kwa muda wa mwaka mzima ili wasiweze kukosa mahudhurio shuleni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad