HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 1, 2022

EU, FAO na Serikali zazindua Kampeni ya Kitaifa ya kuhimiza milo bora zaidi na tabia zinazofaa za lishe nchini

Mkuu wa Rasilimalil za Asili katika Ofisi za Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Lamine Diallo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini leo Aprili, 30,2022, uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT.
Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania, Dkt. Nyabenyi Tipo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini leo Aprili, 30,2022, uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT.*Kampeni ya lishe itahimiza hatua za kukabiliana na utapiamlo nchini

SHIRIKA la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT, zimezindua kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini.

Uzinduzi huo ulikuwa wa aina yake ikiwa Watu 100 wa kwanza kuwasili katika soko la Kisutu leo Aprili 30, 2022 waliangaliwa hali ya lishe kwa kupimwa Uzito na urefu na kuuliszwa aadhi ya maswali kuhusu lishe na kupewa ushauri nini cha kuanya huku wakipewa kikapu cha chakula kilichojaa vyakula anuwai vilivyoonyeshwa katika sahani ya mfano ya milo bora.

Hata hivyo uzinduzi kama huu utazinduliwa Zanzibar Mwezi Mei, mwaka huu kwa kampeni kama hiyo ya lishe ya kitaifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, leo Aprili, 30, 2022 wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Dkt. Honest Kessy, kutoka Wizara ya Kilimo kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa Kilimo na lishe ni sawa na pande mbill za sarafu, na hatuna budi kuimarisha mifumo yetu ya chakula ili kukidhi mahitaji ya lishe ya watu wanaoongezeka kwa kasi duniani.

"Kipaumbele cha serikali ni kupunguza utapiamlo nchini na kampeni hii imekuja katika kipindi mwafaka ambapo dunia inahangaika kumaliza janga la UVIKO-19." Amesema Dkt. Honest Kessy 

Kwa upande wa Mkuu wa Rasilimalil za Asili katika Ofisi za Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Lamine Diallo, amesema kuwa Tanzania itatumia vema fursa ilizo nazo katika kilimo ili kuweza kutatua Changamoyo ya viwango vya juu vya utapiamio katika mikoa kadhaa.

"Kwa dhati kabisa, tunatumaini kwamba kampeni hii ikiunganishwa na shughuli nyingine za AGRI-CONNECT, ambapo itahamasisha na kutoa mchango katika kuimarika kwa kipato cha watu na afya Zao. " Amesema

Kwa upande wa Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania, Dkt. Nyabenyi Tipo, amesisitiza kwamba: "Wakati Janga la dunia likiendelea, umuhimu wa milo bora katika kukabiliana na madhara yake haukuwahi kuwa muhimu zaidi."

Aliongeza kwamba mabadiliko katika tabia za jami kuhusiana na uzalishaji wa chakula, ulaji, na ufufuaji wa masoko utaongeza upatikanaji wa chakula, kuimarisha kinga ya mwili na kuwapa wakulima wadogowadogo kipato.

Programu hiyo inayoongozwa na FAO na inayoitwa "Kujenga Uhimilivu wa Mifumo ya Kilimo na Chakula na Lishe Bora katika Muktadha wa Janga la Dunia ni nguzo ya nne ya mradi wa AGRI-CONNECT- ikiwa ni pamoja na Kusaidia Minyororo ya thamani, uleta Ustawi wa Pamoja unaokazia zaidi lishe na kuanzisha mifumo ya kusaidia kupunguza makali ya janga katika upatikanaji wa chakula na masoko.

"Tumeimarisha usimamizi wetu wa masuala ya lishe kwa kuhimiza uwekezay zaidi katika kilimo, uzalishaji wa chakula, na elimu ya lishe ili kuongeza upatikanaji na ufikiwaji wa milo iliyo bora kupita kuimarisha uzalishaji katika kilimo na uelewa bora zaidi wa umuhimu wa milo bora katika kuzuia matatizo ya afya kwa sababu ya ukosefu wa lishe na kuimarisha kinga ya mwili." Dkt. Nyabenyi Tipo

Kauli mbiu yake ya lishe Bora ni Mtaji kampeni hii ya kitaifa itajumuisha shughuli mbalimbali kama vilie programu za mapishi, Ziara za elimu ya lishe katika dala dala, mafunzo kwa vijana wa kike, na kuanzishwa kwa maeneo ya msosi asilia, ndani ya kipindi cha miaka miwili, kampeni inatarajiwa kuwafikia watu milioni 32 kupitia majukwaa ya kimapokeo na ya mtandaoni.

Uzinduzi huo ulioshuhudiwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Dkt. Honest Kessy, kutoka Wizara ya Kilimo kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Bw. Lamine Diallo, Mkuu wa Rasilimali za Asili katika Ofisi ya Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, na Dkt. Nyabenyi Tipo, Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania, na lilihudhuriwa na watalaamu mbalimbal na wadau katika tukio shirikishi mwambata (mahali halisi na mtandaoni) katika Soko Kuu la Kisutu jijini Dar es Salaam.

Wananchi waliojitokeza kupata huduma leo Aprili, 30,2022 katika soko la Kisutu jijini Dar es Salaam na wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT.
Mwananchi akipata huduma kutoka kwa Maafisa lichi nchini, mara baada ya kujitokeza kupata huduma leo Aprili, 30,2022 katika soko la Kisutu jijini Dar es Salaam na wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT.
Viongozi mbalimbali wakizindua sahani lishe kamili leo Aprili, 30,2022 katika soko la Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT.
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Dkt. Honest Kessy, kutoka Wizara ya Kilimo kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini leo Aprili, 30,2022, uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT.
Mwakilishi kutoka manispaa ya Ilala akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT leo Aprili, 30,2022.
Mbunge Neema Lugangira  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT leo Aprili 30,2022.
Beni ya Msanii Msechu ikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT leo Aprili 30,2022.


Matukio ya lishe yakiendelea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT leo Aprili 30,2022.
Wananchi wakipokea Kapu kwaajili ya kuchukua lishe mhimu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya lishe ili kujenga tabia zinazofaa za milo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana nchini uzinduzi huo umefanywa kwa kushirikiana na Shiriki la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Serikali ya Tanzania, kupitia programu inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) inayojulikana kwa AGRI-CONNECT leo Aprili 30,2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad