Na Amiri Kilagalila,Njombe
BAADHI ya wazee wa kijiji cha Itunduma kata ya Mtwango wilayani Njombe, wamechukizwa na kitendo cha vijana wa kijiji hicho kuacha nyumba na familia zao na kwenda kulala kwenye nyumba za wageni hali inayowapelekea kuwa na maswali mengi juu ya umuhimu wa nyumba hizo kwa wenyeji wa maeneo hayo.
Yenick Mwinami ni mmoja wa wazee wa kijiji hicho katika mkutano wa wananchi,idara ya dawati la jinsia na watoto walipokuwa wakitoa elimu juu ya unyanyasaji wa kijinsia,mauaji pamoja na udumavu ametumia nafasi hiyo kuhoji umuhimu wa nyumba hizo kwa wenyeji.
"Wenzetu wametujengea gesti huko,mimi ni mzee lakini,gesti Ile wamewajengea wenyeji au wamewajengea wageni"alihoji Bi.Yenick Mwinami
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah ametoa wito kwa jamii kurudi kwenye maadili na kuto acha nyumba zao.
"Cha msingi ni kwamba familia mrudi kwenye maadili,msiache familia na kukimbila gest,nyumba mmejenga kwa ajili ya familia zenu"alisema Hamis Issah
Vile vile amewatoa hofu wazee wa kijiji hicho na kudai kuwa nyumba hizo hujengwa sababu mbali ikiwemo wafanyabiashara na wageni wanaofika kwenye maeneo yao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah
No comments:
Post a Comment