HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 12, 2022

WAKALA WA VIPIMO YAHIMIZA UFANYAJI KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA YA VIPIMO, WAFUNGUA MKUTANO MKUU WA MAFUNDI MIZANI DODOMA

Na Mwandishi Wetu - Dodoma
MENEJA wa Survaillance Bw. Almachius Pastory ambaye alimuwakilisha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu amefanya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mafundi Mizani ambao kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kakwe umefanyika Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Almachius Pastory ameeleza kuwa anafarijika sana kuona mafundi wanakuwa na chama ambacho kinazingatia matakwa mbalimbali ya kisheria na miongozo inayotolewa na Serikali hususani swala la uadilifu kwa wadau wa Vipimo ili kupunguza malalamiko kwa Wananchi.

Pia, ameeleza kuwa Viongozi watakao pata nafasi ya kuchaguliwa kuongoza chama hicho watakuwa msaada mkubwa kwetu sote na Taifa kwa ujumla kwani ni viunganishi muhimu kati ya Wakala wa Vipimo na Mafundi wote wanaojishughulisha na urekebishaji na uundaji wa mizani na ukizingatia tunatumia vipimo kufanikisha mambo mbalimbali yanayotuzunguka iwe kwenye ujenzi, Afya, Mazingira, Usalama na katika maeneo yote yanayotuzunguka ya kibiashara.

Kadharika, ameeleza kuwa kipimo ni nyenzo muhimu katika kubadilisha bidhaa na fedha ili biashara ifanyike kwa haki lazima Vipimo sahihi vitumike na muundaji wa Vipimo lazima aunde kipimo chenye usahihi vivo hivyo mrekebishaji wa Vipimo lazima ahakikishe Vipimo vyote vilivyorekebishwa vinakidhi matwakwa ya Sheria ya Vipimo Sura na. 340. Kipimo kisichokidhi matakwa ya kisheria kinaweza kuzidisha au kupunguza uzito wa bidhaa, kuzidisha kunampa hasara mwenye mali au duka na kumfanya asipige hatua katika biashara yake. Kadharika, kupunguza kunasababisha mnunuzi kupata bidhaa pungufu kulinganisha na pesa aliyoitoa.

Vilevile, amewataka mafundi vipimo kuzingatia maadili ya kazi ya ufundi mizani ili kuepukana na adhabu ya faini au vifungo kama Sheria ya Vipimo inavyosema, uzingatiaji wa Sheria utaimarisha uaminifu kwa wateja hivyo kuongeza wigo wa kazi. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa mafundi mizani wenye leseni kwa mwaka huu mpaka sasa ni 274 ambapo asilimia 40 wapo mkoa wa Dar es Salaam.

Hivyo, nichukue nafasi hii kuwahimiza kufungua Ofisi mikoani kwani huko pia wananchi wanahitaji sana huduma zenu kwakuwa kuna Mikoa inaonekana haina fundi hata mmoja jambo ambalo sisawa.

Kwa kumalizia Bw. Pastory kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu ametoa wito kwa mafundi vipimo kujiendeleza kitaaluma ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwakuwa tunakoelekea vipimo vya kidigitali vitachukua nafasi kubwa zaidi ya hivi vinavyotumika sasa hivyo, bila kujiendeleza kazi zetu tutajikuta zinafanywa na wageni kwakuwa hakuna wataalamu wa kuweza kufanya kazi hizo nchini kwetu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mafundi Mizani Bw. Mpasi Kiera akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Mafundi mizani Jijini Dodoma.

Meneja wa Surveillance Bw. Almachius Pastory akipokea Risala kutoka kwa katibu wa chama cha mafundi mizani mara baada ya kumuwakilisha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu katika ufunguzi wa mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa mafundi mizani wakifuatilia Mkutano Mkuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad