HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 19, 2022

USAWA WA KIJINSIA KUCHOCHEA MAENDELEO

 Na Muhammed Khamis

IMEELEZWA kuwa ili Zanzibar iweze kupiga hatua zaidi za kimaendeleo ipo haja ya kukuzwa na kuendezwa usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya famialia na kuendelea.

Kauli hiyo imetolewa na Mkufunzi wa maswala ya kijinsia visiwani hapa Halima Ibrahim wakati alipokua akiwasilisha mada inayolenga umuhimu wa jinsia katika jamii kwa baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya ushirika kutoka maeneo mbali mbali ya Unguja ambao ni wanufaika wa utekelezaji mradi wa Viungo.

Alisema kuwepo kwa usawa wa kijinsia ni nyenzo muhimu ambayo huibua mabadiliko katika jamii na kufanya kuwepo kwa usawa ambao kwa namna moja au nyengine hupelekea huchochea maendeleo ambayo ni hitajio la kila mmoja.

Alisema katika Dunia ya sasa si wakati ambao upande mmoja kweye familia kutegea upande mwengine wakiamini ndio watu wanaopaswa kufanya kazi nyingi zaidi kuliko wao.

Alisema licha ya baadhi ya watu katika jamii kufahamu umuhimu wa jinsia lakini bado Zanzibar kuna baadhi ya familia hazijaona uzito wa jambo hilo muihimu na hadi sasa wanaedelea kuamini kuwa mwanamme ndio mtu pekee ambae anastahili haki zote muhimu kuliko mwanamke.

Alieleza kuwa mazingira yaliopo sasa hakuna haja kabisa ya kuendelea kubaguliwa wanawake ukizingatia wanawake ni watu muhimu na wenye kujiamini kutokana na uwezo mkubwa walionao hivi sasa ukilingamisha na miaka ya nyuma.

Katika hatua nyengine mkufunzi huyo aliwataka washiriki wa mafunzo hayo na wanawake wengine wote kutokuacha kujihusisha na maswala ya kisiasa badala yake wanapaswa kujiweka karibu ka kugombea nafasi za uongozi muda unapofika.

Awali akifungua mafunzo hayo ya siku mbili Afisa uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka TAMWA-ZNZ Nayrat Abdalla Ali alisiema wameamua kuwajengea uwezo wawakilishi hao kutoka vikundi vya ushirika ili elimu hiyo iwafikie wengi zaidi katika vikundi vyao.

Alisema kwa dhana ya kuwaendeleza wanawake kiuchumi hakuna budi wanawake wenyewe kujengwa katika misingi ya kutambua haki zao za kijinsia ambazo wanapaswa kuzipata na kuzifanyika kazi katika maisha ya kila leo.

Mmoja miongoni mwa washiriki hao Khamis Hamad alisema kuna haja kubwa ya elimu ya jinsia kuendelea kutolewa katika maeneo mbali mbali ili kuwafikia walio wengi zaidi na ikiwezekana hata kufundishwa maskulini.

Nae Janet Ovarisit kutokea kianga alisema baadhi ya ndoa zimekua zikikabiliwa na changamoto za ubaguzi wa kijinia zaidi hufanywa na baadhi ya ndugu wa mume ambao mwanamke ameolewa.

Alisema mazingira ya ina hiyo yamekua yakivuruga ndoa nyingi kwa kuwa mke hukosa uhuru kufanya anachokitaka ukizingatia mume wake huwaskiliza zaidi ndugu wa familia yake kuliko mke ambae anaishi nae kwenye ndoa.
Mkufunzi wa maswala kijinsia Zanzibar Halima Ibrahim akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwazo wawakilisho kutoka katika vikundi vya ushrikia ambao ni miongoni mwa wanufaika katika mradi wa viungo,mafunzo ambayo yalifanyika katika moja ya ukumbi wa Wizara ya Afya Mombasa mjini Unguja.
Miongoni mwa washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu umuhimu wa jinsia wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad