HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 7, 2022

Umiliki wa kampuni MIC Tanzania Public Limited Company (Tigo na Zantel) Wakamilika sasa ni Axian telecom na Rostam Aziz

Na Mwandishi wetu

UMILIKI wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania Public Limited Company (Tigo na Zantel) umetangazwa kukamilika baada ya Axian telecom kuungana na Rostam Aziz kwa ajili ya kumamilisha mchakato wa kumiliki Kampuni za mawasiliano za Millicom katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mchakato huo unaleta takribani wateja milioni 14 wa simu za mkononi kwa AXIAN Telecom na kuharakisha ukuaji wa kampuni hiyo barani Afrika

Akizungumzia Muungano wa AXIAN Telecom Mwenyekiti wa AXIAN Telecom Hassanein Hirdjee amesema, Muungano huo umeweka vipaumbele vinne (4) muhimu katika kutekeleza majukumu yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

"Kuendeleza mabadiliko ya kidijitali nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa na kutoa huduma zinazowanufaisha mtumiaji mmoja mmoja na makampuni ya KitanzaNia."

"Kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za mawasiliano na kuongoza ujumuishwaji wa kidijitali kwa kuwekeza kikamilifu kwenye ujenzi wa miondombinu ya mawasiliano."
Aidha amesema "Muungano huu unapanga kuimarisha upatikanaji na ubora wa mtandao hasa kupitia teknolojia ya 4G. Kuongeza kasi ya ujumuishwaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi, kwa kuzingatia mafanikio ya huduma hizi kutoka kwenye kampuni zilizounganishwa ili kuendeleza zaidi huduma za kifedha kwa njia ya simu zinazolenga mahitaji ya wateja wa Tanzania.

Umoja huo pia utahakikisha muungano huu unafaidika kupitia utaalamu wake wa kutoa huduma za kifedha za kiwango cha juu katika nchi zingine.Kukuza na kuendeleza vipaji."

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa "Muungano huo unakusudia kukuza maendeleo ya taaluma za wafanyakazi na kuweka mkazo mkubwa kwenye mafunzo, kubadilishana uzoefu na kushirikishana maarifa ya pamoja miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni iliyounganishwa ya MIC Tanzania PLC.

Mbali na hayo Hirdjee amesema malengo ya pamoja ya AXIAN ni wazi kwamba watafanikiwa kuondoa vikwazo viznavyozuia upatikanaji wa huduma za kidigitali nchini kote;

"Tulipoanza safari yetu ya mawasiliano zaidi ya miaka ishirini iliyopita, suala kubwa lilikuwa kuunganisha watanzania kwenye huduma hii. Tulikuwa waanzilishi katika kujenga mtandao wa huduma za simu, hasa katika maeneo ya vijijini, ambapo kwa sasa Watanzania wenzangu wengi wanafurahia huduma hii.
Tukitazama malengo ya pamoja na AXIAN Telecom, ni Dhahiri kuwa tutafanikiwa kuondoa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa huduma za kidigitali nchini kote, tukizingatia mahitaji muhimu kwa Watanzania na makampuni. "

Kwa upande wake Mwenyekitii MIC Tanzania PLC Rostam Aziz amesema AXIAN ni mkombozi mpya katika kuhamasisha uwekezaji ili kuboresha maisha ya kila siku;

"AXIAN Telecom inafungua njia mpya kwa sekta binafsi barani Afrika kuhamasisha uwekezaji ili kuboresha maisha ya kila siku ya watu inayowahudumia."

Rostam amesema Ikitumia utaalamu wake hasa katika kusambaza teknolojia za hali ya juu kama vile mitandao ya 5G na kuanzisha huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi zilizofanikiwa, AXIAN Telecom ina dhamira ya kuupa nguvu mfumo wa mawasiliano hapa Tanzania hasa katika kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma bora zaidi.

Ikumbukwe kuwa Telecom ni mtoaji wa huduma za mawasiliano barani Afrika wanaofanya kazi katika masoko manane kupitia kampuni tanzu nchini Madagascar, Comoro, Reunion, Mayotte, Senegal, Togo, Uganda na Tanzania Inayofanya kazi katika sehemu tatu kuu za biashara, kutoa huduma za mtandao wa simu na zile zisizotumia mtandao na vile vile miundombinu ya kidijitali na huduma za kifedha kupitia simu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad