HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 26, 2022

SAG YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA MTAMBANI


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Smart Africa Group  (SAG), Emmanuel Kaweda (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula kwa Imam wa Msikiti wa Mtambani, Suleiman Abdallah (wa pili kushoto) na watoto, Abdukalim Yusuf na Samira Said (kulia) vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa watoto yatima wanaolelewa na msikiti huo, Dar es Salaam leo Aprili 26,2022 wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAG Edwin Bruno. KAMPUNI ya Smart Africa Group (SAG, )imetoa msaada wa Vyakula kwa watoto yatima hamsini, wanaosoma kwenye shule ya msingi seminari ya Mtambani jijini Dar es Salaam .


Msaada huo umetolewa leo Aprili 26 2022, na kampuni hiyo zilizokuwa chini ya mwamvuli wa SAG, kwa lengo la kuwafariji watoto hao.

SAG inamuunganiko wa kampuni tano pamoja na :- Smart Codes, Smart Lab, Smart Studio, Smart Nology na Smart Foundry.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Vyakula hivyo, Afisa Mtendaji wa SAG Emmanuel Kawedi amesema kuwa wamewiwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima ambao wanastahili msaada huo kwa kuwa hawana nguzo zao muhimu za kimalezi.

Sheikh Suleiman Abdallah Imam wa Msikiti wa Mtambani pia Mlezi wa shule ya Msingi Mtambani na ile ya Sekondari ya Mvumoni ameishukuru SAG kwa kuwakumbuka watoto yatima waliokuwepo kwenye shule hiyo.

Ameeleza kuwa shule hiyo iliyokuwa chini ya Msikiti wa Mtambani inawanafunzi 300 ambapo wanafunzi 50 ni yatima na ndio waliolengwa kwenye msaada huo.

Amesema kuwa kuwasaidia watoto yatima kunapelekea maisha ya mtoaji kuwa na Baraka .

“Niwape siri moja kuwasaidia watoto yatima kunaongeza Baraka kwenye maisha Mwenyezi Mungu humuondolea matatizo mtu anayewasaidia watoto yatima” amesema Sheikh Abdallah.

Amesema kuwa wanafunzi hao yatima wanasomeshwa kwa sadaka za waumini wanaoswali kwenye msikiti wa mtambani.

Sheikh Abdallah amesema Edwin Bruno ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na muanzilishi wa kampuni hiyo ya SAG ameonesha nia ya kusaidia kuwalipia ada wanafunzi hao tunamshukuru sana.
Mmoja wa watoto yatima wanaolelewa na Msikiti wa Mtambani, Lawwal Mohammed (katikati) akiomba dua kushukuru wafanyakazi wa Kampuni ya Smart Africa Group  (SAG), baada ya kukabidhiwa msaada wa vya kula kwa ajili ya Futari, leo Aprili 26, 2022 jijini Dar es Salaam, kushoto ni Imam wa Msikiti wa Mtambani, Suleiman Abdallah na mtumishi wa SAG, Nawaz James.
Baadhi ya wafanyakazi wa SAG wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima ya shule ya msingi Mtambani Dar es Salaam baada ya kukabidhi msaada wa Vyakula kwa watoto hao leo Aprili 26,2022.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa wa Kampuni ya Smart Africa Group  (SAG), Edwin Bruno (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula kwa Imam wa Msikiti wa Mtambani, Suleiman Abdallah (wa pili kushoto) na watoto, Manal Salum (kulia) na Karim Said vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya watoto yatima yatima wanaolelewa na msikiti huo, Dar es Salaam Aprili 26, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad