HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 4, 2022

Rais Samia azindua na Kugawa Vitendea Kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo nchiniJijini Dodoma leo

 RAIS, Samia Suluhu Hassan azindua na Kugawa Vitendea Kazi mbalimbali kwa Maafisa Ugani Kilimo nchini katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya ukaguzi wa mabanda mbalimbali ya wakulima pamoja na Wafanyabiashara leo tarehe 04 Aprili, 2022 Jijini Dodoma.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Rais Utumishi kupitia upya na kuufanyia mabadiliko muundo wa Tume ya Umwagiliaji ili kuhakikisha inakuwa na Ofisi katika kila Wilaya. 


Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akizindua ugawaji wa vitendea kazi vya maafisa ugani kilimo ikiwemo pikipiki, vifaa vya kupima afya ya udongo, simu janja na visanduku vya ufundi kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.


Aidha, Rais Samia pia ameiagiza Wizara hiyo ishirikiane na Wizara ya Fedha na Mipango, kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo ambao utachangiwa na tozo maalum kwenye mazao ya kilimo, Mfuko Mkuu wa Serikali na wadau wa maendeleo. 


Rais Samia amesema Mfuko huo utakuwa na majukumu ya kugharamia pembejeo za kilimo kama ilivyofanyika kwenye korosho, pamba na tumbaku ili mfuko huo utumike kama ruzuku pindi pembejeo zinapopanda bei. 


Kwa upande mwingine, Rais Samia ameagiza mashamba yote ambayo yapo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kufufuliwa na kuanza kutumika kwa kushirikiana na Sekta binafsi kwa mfumo wa kukodisha ardhi kwa muda mrefu.


Hali kadhalika, Rais Samia ameitaka Wizara ya kilimo kuweka msukumo kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na kuwa ya kibiashara, ikiwemo mazao ya mboga mboga pamoja na mazao ya kimkakati ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza ziada nje ya nchi.


Rais Samia amesema Sekta ya kilimo nchini imeendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa ambapo kwa mwaka 2020 sekta ya kilimo ilikua kwa 4.9 %, kuchangia kwa 26.9% katika pato la taifa, kuchangia kwa 61.1% katika kutoa ajira kwa Watanzania na kuchangia kwa 65% ya malighafi za viwandani. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbalimbali ya zao la mpunga ambao umekobolewa katika viwango mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu na utengenezaji wa nafaka kwa ajili ya mifungo katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za Kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia miche ya matunda ya miembe pamoja na michungwa katika mabanda ya Maonesho ya bidhaa za kilimo nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Taifa Jacqueline Mkindi kuhusu zao jipya la kilimo pamoja na mazao mbalimbali ya Biashara katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akielezea kuhusu vitendea kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo kabla ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu zao la parachichi ambalo limekuwa likiwaletea tija wakulima nchini hususan katika Mikoa ya Njombe, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.

Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 04, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akigawa pikipiki kwa waakilishi wa Maafisa Ugani 7000 katika hafla iliyofanyika nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akigawa pikipiki kwa waakilishi wa Maafisa Ugani 7000 katika hafla iliyofanyika nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Pikipiki Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad