HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 30, 2022

LATRA YATANGAZA NAULI MPYA


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Gilliard W. Ngewe akizungumza na wandishi wa habari pamoja na wadau ikiwemo viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) na Chama cha Wamiliki wa Daladala (TDA) kuhusu nauli mpya za mabasi ya mijini na Mikoani kwenye mkutano uliyofanyika leo katika ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

 
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)  imetangaza nauli mpya za mijini na mikoani ikiwa ni baada ya kukaa na wadau wa usafirishaji kuona ni namna gani wataweza kutoa huduma bora kwa wananchi 

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Gilliard W. Ngewe amesema baada ya kufanya ukokotoaji kwa mujibu wa SHERIA ya LATRA ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 Mamlaka imeridhia na kujiridhisha pia kuweza kuongeza nauli za mikoani na mijini.

Amesema mabasi ya kwenda mikoani kwa daraja la kawaida limeongezeka kwa shilingi 4.40 sawa na asilimia 11.92 ambapo viwango vya kikomo vya zamani kwa abiria kwa kilometa moja ilikuwa ni shilingi 36.89 na sasa viwango ambavyo Mamlaka imeridhia kwa abiria kwa kilometa moja inakuwa shilingi 41.29.

Pia amesema mabasi ya kwenda mikoani kwa daraja la kati limeongezeka kwa shilingi 3.66 sawa na asilimia 6.88 ambapo viwango vya kikomo vya zamani kwa abiria kwa kilometa moja ilikuwa ni shilingi 53.22 na sasa viwango ambavyo Mamlaka imeridhia kwa abiria kwa kilometa moja inakuwa shilingi 56.88.
 
"Viwango vya nauli kwenye barabara za vumbi itakuwa na ongezeko la asilimia 25 ya daraja la kawaida kwa barabara ya lami ambayo ni sawa na shilingi 51.61 kwa abiria kwa kilometa. Alisema Ngewe

Ameongeza kuwa mabasi ya mijini nauli imeongezeka shilingi 100 kama nauli ya mwanzo abiria alikuwa analipa shilingi 400 sasa atalipa shilingi 500 na kama abiria mwanzo alikuwa analipa nauli ya shilingi 750 sasa utalipa shilingi 850.

Awamewasisitiza watoa huduma kwa kuzingatia kanuni ya 19 ya tozo ya LATRA ya mwaka 2020 inayowataka kutoa matangazo ya nauli mpya kwa siku kumi na nne kabla ya kuanza kutumia nauli mpya kupitia vyombo vya habari vinavyoweza kuwafikia watu wengi nchini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad