HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 4, 2022

Kuelekea kongamano la uchangiaji damu, Muhimbili yatakiwa kujitafakari


Mwanafunzi wa akichangia damu wakati wakati wa ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) leo Aprili 4, 2022, Dar es Salaam.

  Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) leo Aprili 4, 2022, Dar es Salaam.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Rifello Sichwele akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) leo Aprili 4, 2022, Dar es Salaam.

Meneja wa Mpango wa taifa wa Damu Salama, Dkt. Magdalena Lyimo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) leo Aprili 4, 2022, Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) leo Aprili 4, 2022, Dar es Salaam.

Picha za Pamoja wakati wakati wa ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) leo Aprili 4, 2022, Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV 
NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa wananchi nchini kujenga tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili kupunguza vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu salama kwa wakati.

Dkt. Molel amesema, huduma ya damu salama ni muhimu ni moja kati ya huduma inayohitajika kwa wingi katika hospitali zote nchini na kwamba damu haiuzwi  wala haitengenezwi zaidi ya watu kujitolea.

Dk Mollel ameyasema hayo leo Aprili 4, 2022,  Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Wiki ya kuchangia damu iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas).

Kuhusu upatikanaji wa damu safi na salama, Dkt. Molel amesema, watazunguka Kanda zote nchini jli kuhakikisha suala la upatikanaji wa damu salama linakuwa siyo tatizo tena hivyo ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupunguza vifo vya mamia ya watu wanaopoteza maisha kwa ukosefu wa damu.

Aidha Dkt. Mollel ametoa miezi miwili kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja ili kupata wateja wengi na kupunguza utegemezi kutoka Serikalini.

Amesema hospitali hiyo ina miundombinu, vifaa bora na wataalamu wakuaminika lakini inakosa huduma kwa wateja jambo ambalo linachangia watu wengi kukimbilia hospitali binafsi.

Amesema, Muhimbili ni suluhisho la matatizo yote ya afya nchini yaliyoshindikana lakini kuna kasoro kubwa ya utoaji wa huduma (Customer care). 

",Wagonjwa wengi wamekuwa wakienda kutibiwa katika hospitali za binafsi lakini pindi wakizidiwa hurudishwa Muhimbili kwa huduma.... hii inaonyesha kuwa, muhimbili ni hospitali bora lakini kasoro yao ni moja tu waboreshe huduma kwa wateja ( customer care).

"Kama  hospitali hii itaboresha huduma kwa wateja kwa kuhakikisha wanawapokea wagonjwa na kuwahudumia vizuri, itapata wagonjwa wengi na kupunguza utegemezi serikali.

"Watu wengi wanaenda kwenda hospitali za binafsi, wanapend kwenda Aghakan lakini wakizidiwa wanaletwa Muhimbili na kuja kuponea hapa, hii ni kwamba Muhimbili kuna wataalamu wazuri shida ni huduma bora kwa wateja, hivyo ushahidi inaonyesha kwamba shida ya watu kwenda kwenye hospitali binafsi wanafuata huduma kwa wateja. Hivyo Muhimbili wanapaswa kuboresha huduma kwa mteja". amesema Dkt. Molel

Aidha Dkt. Molel amewataka madaktari kuwa wabunifu kwa kubuni teknolojia zitakazosaidia kuboresha huduma za afya na kutafiti masuala ambayo hayajulikani ili kuepuka kufanya tafiti za mambo yanayoibuka kila wakati.

Kwa upande wake, Meneja wa Mpango wa taifa wa Damu Salama, Dkt. Magdalena Lyimo amesema ili kukidhi mahitaji ya damu inapendekezwa kwamba, nchi ikusanye Idadi ya chupa za damu sawa na asilimia moja ya wananchi waliopo, hivyo kwa Tanzania tunaitaji chupa 550,000 ili kukidhi mahitaji ya nchi. 

Amesema mpaka sasa nchi ina asilimia 60 tu ya damu  hivyo katika kuziba pengo lililopp inahitajika asilimia 40 ili kufikia mahitaji yanaotakiwa na nchini.

Alisema mwaka 2015 walikusanya chupa 12,597 na mwaka 2021 walikusanya chupa 331,279 na kwamba ongezeko la watu linafanya mahitaji ya damu kuongezeka.

"Uchangiaji wa damu ni wa msimu kuna wakati unaongezeka na wakati mwingine unapungua. Asilimia 87 wanaume ndio wanachangia damu na asilimia 12 ni wanawake. Lakini asilimia 55 ni vijana kati miaka 18 na 29 na asilimia 50 ni wenye damu kundi 0+,’’ ameeleza Dkt Lyimo.

Alisema wanawake ndio kundi linaongoza kwa mahitaji ya damu kwa sababu inahitaji asilimia 30, upasuaji, ajali na watoto na kwamba watu kati ya miaka 15 hadi 44 wanahitaji damu

Naye, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Rifello Sichwele amesema kundi linaloathirika zaidi na kuhitaji damu ni wanawake, watoto, wahanga wa ajali, wenye malaria na saratani hivyo ni vema wizara ikahakikisha kuwa damu salama inapatikana wakati wote.

Amesema elimu ya kutosha itolewe ili kila mmoja aone umuhimu wa kuchangia damu na kumsaidia mtu yeyote ili  damu salama ipatikane kwa wakati na saa 24 katika vituo vyote vya kutolea huduma kwani serikali imenunua vifuko vya kuhifadhia damu.

‘’Kila Mkoa utengeneze mpango wake wa kuhakikisha upatikanaji wa damu salama unafanyika kisha muwasiliane na wizara kwani jukumu lililopo ni kutoa elimu na kuhakikisha damu ipo katika vituo vya kutolea huduma,’’ alisisitiza Dk Sichwele.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha Muhas, Profesa Andrew Pembe amesema Muhas imeona uhitaji wa damu uliopo nchini hivyo iliamua kuwepo kwa wiki hiyo ili kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji.

Profesa Pembe amesema ni lazima watu wafahamu umuhimu na manufaa ya kuchangia damu na kupunguza tatizo.

"Zoezi hili ni sehemu ya maandalizi ya kongamano kubwa litakalofanyika hivi karibuni kuzungumzia saratani ya damu ambayo inapunguza kiasi cha damu mwilini mwa binadamu kwa haraka na kuboresha huduma za matibabu," amesema Pembe

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad