HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 10, 2022

KIJANA HAMAD FAQIHI AIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA 5 KITAIFA YA KUHIFADHI QURAAN TUKUFU

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya Mshindi wa kwanza wa Kuhifadhi Quraan Tukufu katika kundi la waliohifadhi Juzuu 30, Hamad Juma Faqihi (miaka 18) kutoka mkoani Tanga, wakati wa Kilele cha Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tanzania , yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya Mshindi wa pili wa Kuhifadhi Quraan Tukufu katika kundi la waliohifadhi Juzuu 30, Mbarak Othman Ally (miaka 20), wakati wa Kilele cha Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Taasisi ya Istiqaama Muslim Community of Tanzania, yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya  Isitqaama, Sheikh Seif Ally Seif na Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya hiyo, Sheikh Badar bin Sood.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya Mshindi wa kwanza wa Kuhifadhi Quraan Tukufu katika kundi la waliohifadhi Juzuu 10, Ibtisam Bint Hussein Awadh (miaka 15), wakati wa Kilele cha Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Taasisi ya Istiqaama Muslim Community of Tanzania, yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya  Isitqaama, Sheikh Seif Ally Seif na Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya hiyo, Sheikh Badar bin Sood.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubabar Zubeir bin Ally akitoa wasaa wake kwa vijana waliokuwa wakishiki Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Istiqaama Tanzania, yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo akizungumza na kuwahusia vijana walioshiriki Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Taasisi ya Istiqaama Muslim Community of Tanzania, yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya  Isitqaama, Sheikh Seif Ally Seif akizungumza na kuwahusia vijana walioshiriki Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Taasisi ya Istiqaama Muslim Community of Tanzania, yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam.

Vijana walivyokuwa wakichuana katika Mashidano ya 5 Kitaifa ya kuhifadhi Quraan Tukufu, yaliyoratibiwa na Taasisi ya Istiqaama Muslim Community of Tanzania, yaliyofanyika jana kwenye Ukumbi wa NSSF, Ilala jijini Dar es salaam.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad