HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2022

KADI YA NHIF INA HESHIMA KUBWA VITUONI – Dk.Meru

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Dk. Adelhelm Meru akipewa kadi ya NHIF   kutoka kwa Meneja Uhusiano wa NHIF Anjela Mziray wakati  alipotembelea Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mahala Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Dk. Adelhelm Meru akizungumza na waandishi wa Habari wakati alipotembelea Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mahala Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakala Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Dk.Adelhelm Meru ameshuhudia namna Kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya inavyomsaidia yeye na familia yake katika kupata huduma za matibabu.

Amesema bila kuwa na Kadi hiyo angekuwa na mzigo mkubwa sana katika eneo la matibabu hivyo amewaomba wananchi kutofanya mchezo katika kuamua kujiunga na NHIF.

Hayo ameyasema leo wakati alipotembelea banda la NHIF katika viwanja vya CCM Jijini Dodoma kwenye Maonesho ya Wiki ya Usalama Mahala pa Kazi ambapo Mfuko unatoa huduma mbalimbali ikiwemo ya elimu na uandikishaji wa wanachama.

Ameongeza kuwa kadi ya NHIF imekuwa na heshima kubwa katika vituo vyote vya kutolea huduma na kwa sasa imeondoa mitazamo hasi ya kunyanyapaliwa kwa wanachama wa Mfuko.

“Nawasihi sana wananchi wasifanye mchezo na eneo la kujiunga na NHIF kwa sababu maisha ya sasa bila kuwa na bima ya afya ni ngumu sana kumudu gharama za matibabu,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad