HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 6, 2022

IDADI YA WAGONJWA WA SARATANI YAFIKIA 40,000 KWA MWAKA

SERIKALI nchini imewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao hasa kwenye magonjwa yasiyoambukiza hususani Kansa kutokana na idadi ya wagonjwa hao kuongozeka hadi kufikia wagonjwa 40, 000 kila mwaka.

Hayo yamesemwa leo Aprili 6, 2022,. Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Abel Makubi wakati wa kongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS).

Amesema kuwa takwimu zinaonesha wananchi wanaokutwa na maradhi ya saratani wamefikia 40,000 kila mwaka ikiwa hao ni wale ambao wamegundulika kutokana kuwa katika hali mbaya kiafya.

“Tunashauri kila mwaka au kila miezi sita kwa mwenye uwezo afanye uchunguzi wa kuangali afya yake hasa maradhi yasiyoambukiza pamoja na kansa… Kila mwaka tunagundua wananchi 40, 000 wenye matatizo ya kansa na hao ni wale waliojitukoza kupima tu inawezekana wapo zaidi ya idadi hiyo kwa hiyo tunaomba wananchi wajitokeze mapema.” Amesema Makubi.

Amesema kuwa dalili za saratani ziko nyingi kwa hiyo wananchi wasipuuze dalili zozote za ugonjwa au kutojisikia vizuri kiafya.

“Dalili za kansa zipo nyingi, unaweza kupungua uzito, kujisikia homa, kupungikiwa damu au kukohoa damu na matatizo ya tumbo kwa kansa ya tumbo kwa hiyo wananchi wanapojisikia hawako sawa kiafya ni vizuri kwenda kupima mapema ili kujua kama ni ugonjwa wa kawaida au ili upate uhakika kuwa ni ugonjwa wa kawaida ni muhimu kwenda kufanya uchunguzi.” Amesema Makubi.

Amesema kuwa wataalamu mbalimbali wamekutana MUHAS kwa ajili ya kuwasilisha tafiti mbalimbali zinazohusu saratani na kwamba wanalitumia jukwa hilo juu ya kuelemisha wananchi kuhusu kujikinga na magonjwa yasiyoambikiza.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Andrew Pembe amesema kongamano hilo limelenga kutoa matokeo ya utafiti kuelekea kutoa huduma bora za saratani ya damu na mabadiliko ya sera kutokana na mahitaji ya nchi.

‘’Tunatoa wahudumu na wataalamu wa afya ili kusaidia kutoa huduma bora za afya. Tafiti za afya zinafanyika katika maeneeo ya afya yaliyopewa kipaumbele na matokeo ya tafiti hizi tunayasambaza kwa jamii na wanasiasa,’’ amesema Profesa Pembe.

Amesema, wataendelea kutoa elimu, tafiti na tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani ya damu ili kuongeza uelewwa kwa jamii na kubainisha changamoto zinazoikabili nchi katika matibabu ya ugonjwa huo.

Naye, Ahlam Nasser mmoja wa watafiti juu ya maradhi hayo ya saratani ya damu, amesema kuwa wagonjwa wa Saratani hufikishwa Hospitali wakiwa kwenye hatua za mwisho ambapo ni ngumu kupata ufumbuzi wa tiba.

“Saratani ikiwa kwenye hatua ya awali inatibika hivyo natoa wito kwa watanzania kuwahi mapema kwenye uchunguzi” amesema Ahlam.

Mmoja wa wagonjwa waliowahi kuugua Saratani ya damu, Gerard Masalogo amesema kwamba alipona kwa kuwa aliwahi kujifanyia uchunguzi ugonjwa huo ikiwa kwenye hatua za awali.

“Mimi ni miongoni mwa Watanzania waliowahi kupata changamoto hiyo ya Saratani ya damu, kwa sasa naendelea vizuri kwa sababu niliwahi kupata matibabu mapema.” Amesema Masalago.

Amesema kuwa yeye na watu wengine wamesajili taasisi itakayozinduliwa hivi karibu itajihusisha na masuala ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya Saratani damu.

Alipoulizwa kuhusu dalili za ugonjwa huo alijibu kuwa ni ngumu kufahamu dalili hizo kama huna utaalamu wa masuala ya afya hivyo amewasihi wananchi kunda hospitali kwaajili ya kufanyiwa vipimo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Abel Makubi akimpa tuzo ya kutambua mchango wake na kufundisha muda mrefu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas), Dkt. Pius Magesa wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.
Dkt. Pius Magesa akiwa na tuzo yake wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Abel Makubi akimpa tuzo ya kutambua mchango wake na kuandaa mtaala wa kufundishia mpaka sasa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas), Dkt. Hamza Muunda wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.


Picha za pamoja wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Andrea Pembe akizungumza wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Abel Makubi akizungumza wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.
Mmoja wa wagonjwa waliowahi kuugua Saratani ya damu, Gerard Masalogo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.
Baadhi ya Wadau wa afya wakiwa katika ufunguzi wakongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) jijini Dar es Salaam leo Aprili 6, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad