HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 25, 2022

Benki ya CRDB yafutarisha wateja wake na Yatima, Zanzibar

 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akiwakabidhi sehemu ya sadaka ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Muwakilishi wa Kituo cha Wazee cha Barabani, Mzee Ali Hamad Juma,  Unguja Zanzibar ikiwa ni sadaka iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa baadhi ya vituo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki baada ya hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateje wake wa Zanzibar. Katikati ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akiwakabidhi sehemu ya sadaka ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa wawakilishi wa Watoto wanaolelewa katika vituo vya Watoto Yatima vya Mazizini na Assalaam, Unguja Zanzibar ikiwa ni sadaka iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa baadhi ya vituo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki baada ya hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateje wake wa Zanzibar. Katikati ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau wa benki, pamoja na vituo vya watoto yatima na wazee Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mao Zedong na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 450.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wateja, wadau wa benki, pamoja na vituo vya watoto yatima na wazee Zanzibar iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mao Zedong na kuhudhuriwa na zaidi ya watu 450.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad