HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 24, 2022

WAZIRI BITEKO AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA MADINI


Picha ya Pamoja. 

Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza wakati wa kuzindua baraza la wafanyakazi katika mkutano uliofanyika mkoani Morogoro Machi 23, 2022.

 Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru  akizungumza wakati waziri wa Madini alipoungua baraza la wafanyakazi katika mkutano uliofanyika mkoani Morogoro Machi 23, 2022.
.
Baadhi ya wafanyakazi waliohudhulia wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanayakazi katika mkutano uliofanyika mkoani Morogoro Machi 23, 2022.
Waziri wa Madini Dotto Bitteko akifurahiya jambo wakati wa uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi Mkoani Morogoro  Machi 23, 2022.
*Asisitiza watumishi kuepuka vitendo vya rushwa
*Awapongeza kwa maanikio ya wizara
*Awaasa kukufanya kazi kwa uadilifu tuepuke vitendo vya rushwa

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amewapngeza wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mafanikio waliyoyapata, hadi sasa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 406 kwa mwaka huu wa Fedha tunaoendelea kuutekeleza.

Hayo ameyasema wakati wa kufungua baraza la wafanyakazi katika mkutano uliofanyika mkoani Morogoro Machi 23, 2022. Amesema kuwa kilichosababisha mafanikio hayo ni mazingira mazuri ya biashara ya madini pamoja na kuwepo kwa Sheria nzuri ya madini.

Amesema kuwa Sekta ya Madini ni moja ya Sekta ambayo wasipokuwa makini inanyooshewa vidole, hivyo amewaasa kupambana na rushwa kwasababu inadhoofisha utoaji huduma na inaondoa haki kwa wananchi na kuleta manung’uniko katika jamii.

Amesema kuwa Wizara hiyo haitamvumilia mtumishi yoyote atakayebainika na kuthibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

“Hakikisheni mnabeba dhamana ya wizara hii na kutekeleza kikamilifu wajibu wenu kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma na ya utumishi wa umma.” Amesema Biteko

Amesema ushirikishwaji wa watumishi mahali pa kazi unaongeza morali ya kufanya kazi hata hivyo alioji kuwa kabla ya kuwalaumu jiulize unaowaongoza umewapa nini? wanajua mipango? miongozo? Sera? Ilani ya Uchaguzi?

Licha ya hayo amewakumusha baraza la wafanyakazi kufanya tathmini ya miaka mitano (5) ya wizara hiyo tangu kuanzishwa kwake na wasibweteke kwa mafanikio yaliyopatikana pia waangalie viashiria hatarishi vinavyorudisha nyuma wizara.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru amesema kuwa ajenda Kuu katika Mkutano wa Baraza hilo ni kupitia na kujadili utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2021/2022 na kupitia makadirio ya bajeti ya wizara kwa mwaka 2022/2023.

Amesema katika kipindi hiki mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umendelea kuimarika ambapo katika kipindi cha miezi tisa (Januari hadi Septemba 2021) mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la taifa uliongezeka hadi kufikia asilimia 7.3 kutoka mchango wa asilimia 6.5 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2020.

“Katika robo ya Tatu Julai hadi Septemba 2021, Sekta ya Madini imechangia asilimia 7.9 ya Pato la Taifa, Mwelekeo unaonesha kuwa malengo yetu ya kuhakikisha sekta hii inachangia asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyo matakwa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 na Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Taifa yanatekelezeka kila mtu akitimiza wajibu wake.” Amesema Ndunguru.

Amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Februari 2022, wamefanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 404.6, sawa na asilimia 62.6 ya lengo la makusanyo.

Na katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2021 hadi Februari 2022, wizara kupitia Tume ya Madini ilitoa jumla ya leseni 6,382 zikihusisha leseni za utafutaji wa madini, uchimbaji madogo, uchimbaji wa kati, uchimbaji mkubwa, uchenjuaji wa madini, usafishaji madini na biashara ya madini.

Kwa upande wa shirika la Madini nchhini STAMICO amesema shirika hilo limewezesha kutoa mafunzo na huduma mbalimbali kwa wachimbaji wadogo 1,144 waliotembelea vituo vya mfano vya Katente, Lwamgasa na Itumbi.

“Tumeboresha Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.” Amesema

Katika kuboresha ukusanyaji maduhuli, wizara imeanzisha mfumo wa kukusanya maduhuli ya madini ujenzi katika Mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na Dodoma na unatarajiwa kutumika nchi nzima.

Licha ya hayo wizara madini inakabiliwa na changamoto za uwepo wa shughuli za utoroshaji wa madini zinazosababisha upotevu wa mapato ya serikali, uelewa mdogo wa wachimbaji, wafanya biashara wa madini na umma kwa ujumla kuhusu Sheria ya madini, hivyo kusababisha uwepo wa migogoro ya mara kwa mara.

Katika kukabiliana na changamoto hizo, wizara imeweka mikakati na hatua mbalimbali ya kukabiliana nazo ikiwemo kuimarisha usimamizi wa shughuli za madini na ukusanyaji wa mapato ya serikali yatokanayo na rasilimali madini kwa kushirikisha mamlaka mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad