Vivo Energy yazindua kampeni Ya Jaza Ushinde na Engen - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 10, 2022

Vivo Energy yazindua kampeni Ya Jaza Ushinde na Engen

 Makamu wa Rais Mtendaji wa Vivo Energy Kanda ya Mashariki na Kusini, Hans Paulsen aliwashukuru wateja kwa ushirikiano wao katika mwaka wa kipekee wa 2021 uliowezesha Engen Tanzania kukuza vituo 20 zaidi mwaka 2021, na kuwashukuru kwa ushirikiano wao katika miezi michache ya kwanza ya 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vivo Energy Tanzania Bi. Khady Sene akizungumza na wageni waalikwa na wanahabari wa kati wa uzinduzi wa promsheni ya 'Jaza Ushinde na Engen' yenye nia ya kurudisha shukrani kwa wateja wao.
Meneja Mauzo Mkazi wa Kampuni ya Vivo Energy Tanzania Eng. Shaaban Kayungilo akizungumza na wageni pamoja na wanahabari

Moja ya zawadi atakayojishindia mshindi atakayeshinda Bahati Nasibu ya 'JAZA USHINDE NA ENGEN'
Ukaribisho kwa Wageni waliohudhuria katika uzinduzi wa promosheni ya 'Jaza Ushinde na Engen'
Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia uzinduzi huo.
 Makamu wa Rais Mtendaji wa Vivo Energy Kanda ya Mashariki na Kusini, Hans Paulsen na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vivo Energy Tanzania Bi. Khady Sene wakikata utepe kuzindua promsheni ya 'Jaza Ushinde na Engen' yenye nia ya kurudisha shukrani kwa wateja wao.
Makamu wa Rais Mtendaji wa Vivo Energy Kanda ya Mashariki na Kusini, Hans Paulsen akijazia mteja mafuta ikiwa ni ishara ya kuzindua promsheni ya 'Jaza Ushinde na Engen' yenye nia ya kurudisha shukrani kwa wateja wao.

Kampuni ya Vivo Energy Tanzania, inayosambaza na kuuza mafuta yenye chapa ya Engen na Shell nchini, imezindua promosheni ya kitaifa ya wateja wake iliyopewa jina la 'Jaza Ushinde na Engen'.

Jaza Ushinde na Engen imeweza kutafuta njia mbadala ya kuweza kuwashukuru  wateja wao kwa hii wanavyofanya manunuzi ya mafuta katika vituo vyao vya kujaza mafuta nchini. Ofa hiyo itaendelea kwa muda wa wiki nane. AmbapItafungwa tarehe 9 Mei 2022.

Njia ya kuingia kwenye ofa itakuwa kupitia droo ya bahati nasibu. Ambapo wateja watapokea kuponi wanaponunua petroli au dizeli katika viwango vilivyo hapa chini kwa kila gari:

• Bodaboda na Bajaj: Tsh. 10,000

• Magari Binafsi: Tsh. 50,000

• Daladala, Malori na mabasi yaendayo mikoani: Tsh. 100,000

Kisha wateja watahitajika kujaza kuponi, kuambatisha nakala ya risiti ya muamala na kuingia kwenye kisanduku cha bahati nasibu ndani ya kituo, na kuondoka na sehemu ya kuponi kwa ajili ya kuthibitishwa ikiwa utawasiliana naye kama mshindi.

Kutakuwa na droo mbili za kila mwezi. Ambapo awamu ya kwanza ya washindi watajishindia Fridges na TV na droo nyingine kuu mwezi Mei, ambapo washindi watajishindia aidha Pikipiki za Boxer BM125, Fridges, TV Flat Screen au zawadi nyingine nyingi.

Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni hiyo, Makamu wa Rais Mtendaji wa Vivo Energy Kanda ya Mashariki na Kusini, Hans Paulsen aliwashukuru wateja kwa ushirikiano wao katika mwaka wa kipekee wa 2021 uliowezesha Engen Tanzania kukuza vituo 20 zaidi mwaka 2021, na kuwashukuru kwa ushirikiano wao katika miezi michache ya kwanza ya 2022.

Mbali na kuelezea faida za bidhaa na huduma zetu, kama Kampuni tuna nia ya kuwezesha ujasiriamali kwa wateja wetu na kwa hivyo tunaamini kuwa zawadi za Jaza Ushinde na Engen zitasaidia sana katika kukuza maisha yao ya kiuchumi” alisema Hans Paulsen. .

Vivo Energy Tanzania inajivunia kutoa bidhaa na huduma bora zaidi za Engen nchini. Hizi ni pamoja na mafuta ya Engen na  Shell; utaalamu unaoongoza katika sekta ya teknolojia na kiufundi; na huduma ya kibinafsi iliyojitolea kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad