Serikali yawaonyo wazalishaji bidhaa bandia
Na Karama Kenyunko
SERIKALI imetoa agizo kwa wazalishaji wa vinywaji vikali bandia nchini, kurasimisha bidhaa zao na kutoa onyo kwa wale ambao wataenda kinyume na agizo hilo.
Hayo yamesemwa leo Machi 16, 2022 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na biashara katika kiwanda cha Konyagi nchini TDL).
Amesema kuwa wazalishaji watakaozalisha bidhaa hizo zisizorasimishwa watachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wamekuwa wakiikosesha serikali mapato.
“Sisi kama Wizara tutahakikisha wale ambao wanazalisha vinywaji hivi vikali nje ya utaratibu tutawasaidia warasimishe lakini wale watakaoendelea na uzalishaji wa bidhaa bandia watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwakamata na kuharibu bidhaa hizo zinazouzwa kwa njia ya panya”,
“Tunautaratibu wa kusimamia wazalishaji ili wazalishe kwa tija na wasaidie uchumi wa nchi” ameeleza Naibu Waziri Kigahe.
Aidha ametoa wito kwa wazalishaji kuwaunga mkono wakulima kwa kununua malighafi kutoka kwao na kuwageukia wakulima pia kuzalisha bidhaa zao kwa njia ya kisasa na kwa wingi zaidi.
Kwa upande wake David Kihenzile Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya viwanda na Biashara na pia Mbunge wa Mufindi Kusini , amesema kuwa kamati hiyo ipo kwenye zaira ya kutembelea viwanda , taasisi mbalimbali zinazohusu biashara na mazigira, na kwamba wamefiki kwenye kiwanda cha TDL kwa ajili ya kuona uzalishaji na changamoto zao.
Amesema kamati hiyo imesikia kilio cha wazalishaji hao kuwa bidhaa bandia zinazouzwa mitaani imekuwa kikwazo kwenye bidhaa zao.
Amesema wamemewasikia TDL wakidai kuwa takribani Asilimia 55 ya bidhaa zinazouzwa mitaani ni bandia .
“Kama kweli hali ipo hivyo ni hatari na kwamba serikali inakosa karibia Shilingi 1.2 Trilion za kodi kwa mwaka mmoja…ukisikia hivyo unawaza kiasi hicho kingejenga barabara ngapi, vituo vya afya vingapi tungepata dawa kiasi gani kwa unaona madhara yake” Amesema Kihenzile.
Amesema kuwa Kamati hiyo imemuomba Waziri achukulie uzito suala hilo na kwamba serikali iwashauri wazalishaji bidhaa bandia kuacha kitendo hicho.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TDL Mesia Mwangoka ameoimba Serikali kutengeneza adhabu ngumu zaidi ili wale wote wanaohusika na kutengeneza bidhaa bandia wasiweze kuendelea kufanya hiyo biashara.
"Tunaomba serikali kutunga sera kali zaidi kwani sera za sasa hivi zinamuwezesha yule anayetengeneza bidhaa bandia kuendelea na biashara yake, faini zake ni ndogo sana unakuta mtu anazalisha bidhaa bandia ya milioni mia mbili, faini yake analipa milioni mbili lazima aendelee kuzalisha kwa sababu haoni hasara kwa kuwa adhabu anayopewa ni ndogo sana na haimfanyi yeye kuvunja ile biashara", amesema Mwangoka.
“Tumefanya utafiti Mwaka jana sisi kama TDL kupitia wakaguzi inaonyesha serikali inapoteza kwa mwaka takribani Trilioni 1.2 kutokana na bidhaa bandia zilizopo mtaani” amesema Meseia.
Lengo kubwa la Kamati kwenda TDL ni kuangalia namna gani ya kutatua tatizo la bidhaa bandia huko mitaani, Wameangalia serikali inaweza kufanyaje kutatua tatizo hilo na imeonyesha nia ya kusaidia kiwanda hicho
Amesema kuwa TDL inajitahidi kupanua soko la uzalishaji wa wine na inampango wa kuongeza nguvu kwenye kilimo cha Zabibu na kwamba wameiambia kamati hiyo kulitazama suala hilo kisera.
8-Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TBL, Mesiya Mwangoka, akielezea jambo kwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara walipotembelea Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distliers Ltd (TDL) , Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment