HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 25, 2022

Serikali imezundua vipaumbele vya kitaifa vya tafiti mwaka

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia,  Omari Kipanga akizungumza na Dkt. Amos Nungu wakati wa uzinduzi wa vipaumbele vya utafiti kwa mwaka 2021/22-2025/26. Miongozo hiyo ni ya uanzishaji na uendeshaji wa kamati za kusimamia.  Maadili ya utafiti na mwongozo wa kitaifa wa uanzishaji na uendeshaji wa voda vya utafiti nchini leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia,  Omari Kipanga (kushoto) akizindua vipaumbele vya utafiti kwa mwaka 2021/22-2025/26. Miongozo hiyo ni ya uanzishaji na uendeshaji wa kamati za kusimamia.  Maadili ya utafiti na mwongozo wa kitaifa wa uanzishaji na uendeshaji wa voda vya utafiti nchini. Mwenye suti nyeusi katikati ni Profesa Yunus Mgaya, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia,  Omari Kipanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa vipaumbele vya utafiti kwa mwaka 2021/22-2025/26. Miongozo hiyo ni ya uanzishaji na uendeshaji wa kamati za kusimamia.  Maadili ya utafiti na mwongozo wa kitaifa wa uanzishaji na uendeshaji wa voda vya utafiti nchini. Pembeni ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania,  Anders  Sjoberg, aliyeinama ni Profesa Mdoe, Naibu Katibj Mkuu, wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akifuatiwa na Mkurugenzi wa Costech, Dkt. Amos Nungu leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Wadau mbali mbali wa tafiti za Sayansi, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia,  Omari Kipanga wakati wa uzinduzi wa vipaumbele vya utafiti kwa mwaka 2021/22-2025/26. Miongozo hiyo ni ya uanzishaji na uendeshaji wa kamati za kusimamia.  Maadili ya utafiti na mwongozo wa kitaifa wa uanzishaji na uendeshaji wa voda vya utafiti nchini. leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia,  Omari Kipanga wakiurahia jambo mara baada ya uzinduzi wa vipaumbele vya utafiti kwa mwaka 2021/22-2025/26. Miongozo hiyo ni ya uanzishaji na uendeshaji wa kamati za kusimamia.  Maadili ya utafiti na mwongozo wa kitaifa wa uanzishaji na uendeshaji wa voda vya utafiti nchini leo Machi 25, 2022 jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI imezindua vipaumbele vyake vya kitaifa vya tafiti kwa mwaka 2021/22-2025/26 ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kamati ya maadili ya utafiti na mfumo wa kitaifa wa wenyeviti wa utafiti kwa lengo la kuhakikisha inakuza na kudumisha ubora wa tafiti nchini.

Juhudi hizo za uzinduzi wa vipaumbele hivyo nikuhakikisha kunakua na matokeo yenye tija zaidi katika tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, Naibu Waziri Omari Kipanga alisema tume imeratibu uanzishwaji wa miongozo ya uundaji na uendeshaji wa kamati za kisekta za kusimamia maadili ya tafiti nchini katika taasisi nne za kisekta kutoka Tanzania bara.

Alizitaja kuwa ni Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (Taliri) na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori) huku kwa Zanzibar ni pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (Zari), mifugo Zanzibar, Taasisi ya utafiti (Zaliri), Zahri na Zafiri.

“Ili kuendeleza na kukuza sayansi na teknolojia nchini Serikali pia imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha taasisi za elimu ya juu pamoja na zile za utafiti na maendeleo zinazoshirikiana na taasisi za kimataifa katika nyanja za teknolojia ya sayansi na ubunifu,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha mwongozo wa taifa wa utafiti wa maadili unatekelezwa na wadau wa utafiti, tume imeratibu uandaaji wa miongozo ya kitaifa ya uanzishaji na utekelezaji wa kamati za maadili za utafiti.

Kwa mujibu wake, lengo ni kuhakikisha tafiti zote zinazofanywa nchini zinazingatia maadili ya tafiti zikiwemo sheria, kanuni na taratibu ili kuongeza tija na kukuza uchumi wa nchi.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk Amos Nungu alisema Tume kwa kushirikiana na taasisi za utafiti na Vyuo Vikuu iliandaa miongozo hiyo mitatu kwa kuzingatia nyaraka mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

“Miongozo hiyo ni pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano III, 2021/22-2025/26,” alisema.

Alisema uamuzi wa kuandaa miongozo hiyo ni matokeo ya Tanzania kushinda nafasi mbili za wenyeviti wa utafiti ambazo zinafadhiliwa na Oliver Thambo huko Afrika Kusini.

Katika hatua nyingine, Balozi wa Sweden nchini, Andre's Sjöberg alisema kuwa Sweden inaamini kuwa nchi zote zinahitaji msingi sahihi wa utafiti.

"Utafiti hautoi maarifa na uvumbuzi mpya pekee, unatoa zana za kushughulikia maarifa kwa utaratibu," alisema.

Alisema watafiti wa Tanzania wanaweza kupata tafiti za kimataifa na wanaweza kutafsiri maarifa yaliyopo ambayo yanaweza kutumika kuelewa na kuchambua hali na mazingira ya eneo husika.

Alisema uwekezaji katika utafiti hulipa kwa sababu ni wazi kuwa utafiti na uvumbuzi ni mambo muhimu ya kushughulikia maswala ya kijamii. “Tunatakiwa kuhakikisha tuna zana sahihi za kutekeleza utafiti,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad